Yanga imefanikiwa kupitisha jina la mshambuliaji wa zamani wa Zesco, Winston Kalengo.
Kalengo ametua Yanga baada ya jina lake kuwasilishwa katika nusu saa ya mwisho kabla ya dirisha ya usajili.
Taarifa zinaeleza, Yanga imepitisha jina hilo la Kalengo anayechukua nafasi ya Mzambia, Obey Chirwa.
Yanga
imemrudisha Chirwa FC Platnums kwa mkopo, safari hii akiwa analipwa
nusu mshahara na Yanga na Wazimbabwe hao watamlipa nusu mshahara.
Mjadala
mkubwa kuhusiana na hilo, ndiyo ulichelewesha Yanga kuwasilisha jina
hilo katika hatua za mwisho na imeelezwa Yanga wameliwasilisha katika
majina ya wachezaji wao saa 5:36, ikiwa ni dakika 24 kabla ya usajili
huo wa dirisha dogo kufungwa.
Pamoja
na kufanya vizuri Zambia akiwa na Zesco, Kalengo aliwahi kucheza soka
la kulipwa nchini Congo Brazaville na anaelezwa kuwa mkali wa kupiga
mashuti, mwenye njaa ya mabao.
Chanzo: Saleh Jembe
Chanzo: Saleh Jembe
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni