TUZO ZA BBC;
Riyad Mahrez ametawazwa kuwa Mwanakandanda Bora wa Afrika wa BBC wa Mwaka 2016.
Mashabiki kutoka kila pembe ya
dunia walimpigia kura nyingi kiungo huyu wa kati wa Algeria na Leicester
kuliko Pierre-Emerick Aubameyang, Andre Ayew, Sadio Mane na Yaya Toure.
Mahrez ameambia BBC Sport: “Naam,
[tuzo hii] ina maana kubwa sana kwa sababu bila shaka mimi ni Mwafrika
na ni jambo kuu sana kwa mchezaji wa Afrika nafikiri, kwa hivyo nina
furaha isiyo na kifani, najivunia kuipokea..”
Tuzo hii ni kilele kwenye mwaka
mzuri kwa mchezaji huyu wa miaka 25, ambaye tayari amejishindia taji la
Ligi ya Premia na alishinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka chaguo la
Wachezaji Uingereza.
Mahrez ametambuliwa kwa uchezaji
wake mzuri kama mchawi katika wingi, ambaye familia yake inatoka kijiji
kidogo kwa jina El Khemis nchini Algeria, ambaye alitikisa Ligi ya
Premia.
Alisaidia sana Leicester City
kushinda ligi bila kutarajiwa, ambapo alifunga mabao 17 na kusaidia
ufungaji wa mabao 11 kuwawezesha kushinda, licha ya uwezekano wao
kushinda mwanzoni mwa msimu kuwa 5000-1 pekee.
Mwezi Mei, Mahrez aliibuka
Mwafrika wa kwanza kuteuliwa mchezaji bora zaidi ligi na wachezaji
wenzake, miaka miwili tu baada yake kujiunga na Leicester kutoka Le
Havre kwa £400,000.
Ni ufanisi mkubwa kwa mchezaji
huyu aliyeanza maisha akicheza soka katika barabara za mtaa alipokuwa
mtoto ambaye sasa amekuwa nyota anayeshindana na wachezaji bora zaidi
duniani katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Amefunga mabao manne katika mechi
tano alizocheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, ishara kwamba anaweza
kutamba hata katika ligi zenye ushindani mkubwa zaidi.
Amefana pia akicheza soka ya
kimataifa Katika mechi tano alizochezea Algeria, amefunga mabao mawili
na kusaidia ufungaji wa magoli matano, na akawezesha Mbweha hao wa
Jangwani kufuzu kwa fainali za Kombe la Taifa Bingwa Afrika mwezi ujao.
Kadhalika, ufanisi wake
umetambuliwa na shirikisho la soka duniani FIFA, ambao walimuorodhesha
kwenye orodha ya wachezaji watakaoshindania tuzo ya Mchezaji Bora wa
Mwaka Duniani – Mwafrika pekee katika orodha ya wachezaji 23.
Mahrez sasa anajiunga na vigogo wa
soka Afrika , wakiwemo Abedi Pele, Jay-Jay Okocha na Didier Drogba,
ambao wamewahi kushinda Tuzo ya BBC ya Mwanakandanda Bora wa Afrika wa
Mwaka.
Na ikizingatiwa kwamba bado ana
miaka mingi ya kucheza, bado kuna muda kwake Mahrez kuwafurahisha
mashabiki, ambao wameonesha jinsi wanavyompenda.
WASHINDI WALIOPITA WA BBC;
TUZO ZA BALLON D'OR
Mshabuliaji wa Real
Madrid amefunga mwaka kwa style ya pekee huku umri ukionekana kuelekea
ukingo kwani mwaka huu amefunga magoli mawili ya Uefa Champions ila ndo
mshindi wa Ballon d’Or.
Maana amefanikiwa
kushinda tuzo ya mwanasoka bora wa dunia maarufu kama Ballon d’Or .
Ronaldo sasa anaichukua mara ya nne, akiwa alianza mwaka 2008 akiwa
Manchester United na alipoingia Madrid, unaweza kusema hii ni ‘hat
trick’.
Kabla haijawa Ballon d’Or, Ronaldo alichukua mwaka 2008, Messi akachukua mwaka 2009.
Baada ya kuwa Ballon d’Or, Messi amechukua mara nne miaka ya 2011, 2012, 2013 na 2015. Huku Ronaldo akiwa amechukua mara tatu katika miaka ya 2013, 2014 na 2016.
Baada ya kuwa Ballon d’Or, Messi amechukua mara nne miaka ya 2011, 2012, 2013 na 2015. Huku Ronaldo akiwa amechukua mara tatu katika miaka ya 2013, 2014 na 2016.
Kumbuka alishinda Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Real Madrid, akashinda Kombe la Euro akiwa na Ureno.
KURA ALIZOZIPATA RONALDO NA WASHINDANI WENGINE PIA WASHINDI WA MIAKA YA NYUMA;
Nyota wa Barcelona Andres Iniesta hajapata hata kura moja katika tuzo za mwaka huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni