Goli la nahodha wa Azam Azam FC John Raphael
Bocco limetosha kuipatia pointi tatu muhimu Azam FC mbele ya Simba SC katika
mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Taifa hii leo.
Katika mchezo wa leo wa ligi kuu ya vodacom ulishuhudia timu zote zikienda mapumziko zikiwa sare ya bila kufungana, huku pande zote mbili zikishambuliana kwa zamu.
Katika kipindi cha pili kocha wa Azam FC, Iddi Nassoro Chechealifanya mabadiliko ya kumtoa Ramadhani Singano na kuingia Yahya Muhammed, huku Kocha wa Simba Joseph Omog akimuingiza Ibrahim Ajib.
Mabadiliko hayo yalipelekea muda mwingi Simba Sc kuwa langoni kwa Azam FC, wakati Azam wakitumia mashambulizi ya kushtukiza na mnamo dakika ya 70 John Bocco aliiandikia Azam FC goli la ushindi.
Kuingia kwa goli la Bocco klipoteza utulivu kwa Simba Sc na kama Azam FC wangekuwa makini ndani ya dakika 5 baada ya kufunga goli walikuwa na uwezo wakupata goli la pili, hadi dakika 90 zinamalizika Azam FC walikuwa mbele kwa goli 1-0.
Kikodi cha Simba SC leo kilikuwa; Daniel Agyei, Janvier Bokungu/Ibrahim
Hajib dk59, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Abdi Banda, Method Mwanjali, Jonas
Mkude, Said Ndemla, Jamal Mnyate/Shiza Kichuya dk47, Muzamil Yassin, Pastory
Athanas na Juma Luizio/Laudit Mavugo dk65.Katika mchezo wa leo wa ligi kuu ya vodacom ulishuhudia timu zote zikienda mapumziko zikiwa sare ya bila kufungana, huku pande zote mbili zikishambuliana kwa zamu.
Katika kipindi cha pili kocha wa Azam FC, Iddi Nassoro Chechealifanya mabadiliko ya kumtoa Ramadhani Singano na kuingia Yahya Muhammed, huku Kocha wa Simba Joseph Omog akimuingiza Ibrahim Ajib.
Mabadiliko hayo yalipelekea muda mwingi Simba Sc kuwa langoni kwa Azam FC, wakati Azam wakitumia mashambulizi ya kushtukiza na mnamo dakika ya 70 John Bocco aliiandikia Azam FC goli la ushindi.
Kuingia kwa goli la Bocco klipoteza utulivu kwa Simba Sc na kama Azam FC wangekuwa makini ndani ya dakika 5 baada ya kufunga goli walikuwa na uwezo wakupata goli la pili, hadi dakika 90 zinamalizika Azam FC walikuwa mbele kwa goli 1-0.
Azam FC; Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gardiel Michael, Yakubu Mohammed, Aggrey Morris, Stephan Kingue/Mudathir Yahya dk77, Himid Mao, Joseph Mahundi, Frank Domayo, John Bocco/Abdallah Kheri dk83 na Ramadhani Singano ‘Messi’/Yahya Mohammed dk63
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni