Shirikisho la Soka nchini, TFF limetoa ratiba ya raundi ya sita ya Kombe la Shirikisho inayotarajiwa kuchezwa kuanzia Februari 24 hadi Machi 7 mwaka huu.
Ratiba hio inaonesha Azam itacheza na Mtibwa Sugar Februari 24 katika uwanja wa Chamazi. Kagera watakuwa wenyeji wa Stand United katika dimba la Kaitaba, Bukoba.
Mighty Elephants ambayo ni kati ya timu mbili za Ligi Daraja la Pili zilizosalia mashindano itakuwa mwenyeji wa Ndanda katika uwanja wa Majimaji.
Timu nyingine ya Ligi Daraja la pili, Madini imepangwa kucheza na JKT Ruvu wakati Mbao na Toto Africans zitamenyana katika uwanja wa CCM Kirumba.
Mahasimu wa jiji la Mbeya, maafande wa Prisons na Mbeya wataamsha tena upinzani wao kwa mechi ya tatu msimu huu.
Machi Mosi, Simba waliotolewa katika hatua ya robo fainali msimu uliopita watakuwa na mtihani wa kupambana African Lyon ambao walitibua rekodi ya wekundu wa Msimbazi kutopoteza mchezo huu walipogonga bao 1-0 bila katika mchezo wa Ligi Kuu.
Mabingwa watetezi Yanga watakamilisha ratiba ya raundi kwa kuwavaa Kiluvya United ya dirisha la Kwanza Machi 7 katika uwanja wa Taifa, jijini Dar.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni