Kikao cha Bodi ya
Kusimamia na Kuendesha Ligi, kiliketi mwanzoni mwa wiki hii na kufanya tathmini
ya mambo mbalimbali yaliyotokea kwenye michezo mbalimbali ya mpira wa miguu kwa
michuano yote – Ligi Kuu ya Vodacom, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili.
Haya haya ndiyo
yaliyojiti katika kila mchezo.
Mechi namba 170 (Stand United FC vs Majimaji). Majimaji iliwasilisha malalamiko kuwa
chumba chao kubadilishia nguo (changing room) kilipuliziwa na timu pinzani dawa
ambayo ni sumu, hivyo kushindwa kukitumia wakati wa mapumziko.
Klabu ya Stand
United FC pamoja na Meneja wa Uwanja waandikiwe barua kuwa vitendo hivyo
vikiendelea kujitokeza uwanja huo utafungiwa kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom.
Msimamizi wa
Kituo aandikie taarifa yake (report) kuhusu tukio hilo. Pia Daktari wa Uwanja,
Dk. Abel Kimuntu awasilishe taarifa yake ya kitaalamu kuhusu suala hilo,
vilevile Meneja wa Uwanja huo, Meja mstaafu Mohamed Ndaro naye awasilishe
taarifa yake kuhusu tuhuma hizo za kumwaga dawa kwenye vyumba.
Mechi namba 173 (Ruvu Shooting vs Azam). Klabu ya Ruvu Shooting iandikiwe barua
kuhusu ubovu wa uwanja wake eneo la kuchezea (pitch) ambapo kuna mashimo, hivyo
wafanyie marekebisho.
Ligi Daraja la Kwanza
Mechi namba 49 (Polisi Morogoro vs Kinondoni
Municipal Council FC). Klabu ya Polisi Morogoro imepigwa faini
ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa kuchelewa kufika uwanjani kwa dakika 20, kitendo
ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(9) ya Ligi Daraja la Kwanza. Adhabu hiyo
imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(48) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Mechi namba 52 (Mbeya Warriors vs Njombe Mji). Mchezaji Boniface S. Nyagawa wa Mbeya
Warriors amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa
kutoa lugha ya matusi kwa Mwamuzi Msaidizi Namba Moja, tukio lililosababisha
atolewe kwenye benchi kwa kadi nyekundu. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia
Kanuni ya 37(7).
Mechi namba 49 (Polisi Mara vs Singida United
FC). Mwamuzi Msaidizi Namba Moja, Enock Mwanyonga, na Mwamuzi
Msaidizi Namba Mbili, Abdulaziz Ally wameondolewa kwenye orodha ya waamuzi wa
Ligi Daraja la Kwanza baada ya kushindwa kumudu mchezo huo.
Uamuzi huo
umefanywa kwa mujibu wa Kanuni ya 38(1a) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu
Udhibiti wa Waamuzi.
Mechi namba 56 (Singida United vs Alliance
Schools FC). Mwamuzi Msaidizi Namba Moja, Omari
Miyala, na Mwamuzi Msaidizi Namba Mbili, Innocent Mwalutanile wamefungiwa miaka
miwili kwa kushindwa kumudu mchezo huo. Uamuzi dhidi yao umezingatia Kanuni ya
38(1a) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.
Naye Kamishna
Hamisi Kambi ameondolewa kwenye orodha ya Makamishna wa Ligi Daraja la Kwanza
kwa kushindwa kutoa taarifa ya mchezo huo kwa usahihi. Adhabu hiyo imetolewa
kwa kuzingatia Kanuni ya 39(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa
Kamishna/Mtathmini Waamuzi.
Klabu ya
Alliance Schools FC imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kugoma
kuinbia kwenye chumba vya kubadilishia (changing room), hivyo kusababisha timu
yako ikaguliwe kwenye gari. Adhabu imezingatia Kanuni ya 14(48) ya Ligi Daraja
la Kwanza.
Ligi Daraja la Pili
Mechi namba 27 (Bulyanhulu FC vs Mashujaa). Klabu ya Bulyanhulu FC imepigwa faini ya
sh. 300,000 (laki tatu) baada ya timu yake kuchelewa kufika kwenye kikao cha
maandalizi ya mechi (pre match meeting). Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya
14(3) ya Ligi Daraja la Pili.
Waamuzi wa mechi
hiyo; Mwamuzi Elikana E. Mhoja (Mwanza), Mwamuzi Msaidizi Namba Moja, John
Mrisho (Mwanza), na Mwamuzi Msaidizi Namba Mbili, Mukhusin I. Abdallah wa
Mwanza wameondolewa kwenye orodha ya waamuzi kwa kushindwa kumudu mchezo huo.
Uamuzi dhidi yao umezingatia Kanuni ya 38(1a) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu
Udhibiti wa Waamuzi.
Pia timu ya
Bulyanhulu FC ilichelewa kufika kwenye kikao hicho katika mechi namba 28 dhidi
ya Milambo FC iliyofanyika kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, mjini Tabora.
Mechi namba 30 (Mawenzi Market vs Sabasaba
United). Klabu ya Mawenzi Market imepigwa faini
ya sh. 100,000 (laki moja) kwa kufika kwenye kikao cha maandalizi ya mechi (pre
match meeting) ikiwa na maofisa wawili tu badala ya wanne, na pia kutokuwa na
vifaa vya mchezo. Adhabu dhidi ya klabu ya Mawenzi Market imetolewa kwa
kuzingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Pili.
Mchezaji Awadh
Ahmed wa Sabasaba United amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000
(laki tano) kwa kumsukuma Mwamuzi na kugoma kutoka uwanjani baada ya kuonyeshwa
kadi nyekundu. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 37(7) ya Ligi Daraja la
Pili kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.
AJENDA 79/MSC/2017- MALALAMIKO YA ALLIANCE
SCHOOLS
Malalamiko ya Alliance
Schools FC kupinga matokeo ya mechi yake dhidi ya Singida United kwa madai
mabao mawili waliyofungwa si halali, na mchezo huo urudiwe kwenye uwanja huru
(neutral) yametupwa.
Msingi wa kutupa
malalamiko hayo ni kuwa matokeo ya uwanjani hayawezi kubadilishwa kwa sababu ya
kupinga mabao yaliyofungwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni