Vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wamefanikiwa kutinga fainali ya kombe la Shirikisho baada ya kuwaondosha mashindanoni wanafainali wa msimu uliopita, Azam wa kwa ushindi wa bao 1-0.
Bao pekee na la ushindi kwa Simba lilifungwa na Mohamed Ibrahim aliyemalizia krosi ya Laudit Mavugo ya dakika 48.
Simba wangeondoka na ushindi mnono kama wangeweza kutengeneza na kuzitumia kufuatia Azam kucheza pungufu toka dakika ya 16 pale Abubakar Salum alipotolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kumchezea vibaya Ibrahim Ajib.
Licha ya upungufu huo na kuonekana kuzidiwa eneo la katikati, Azam walitengeneza nafasi kadhaa za wazi lakini Shaban Idd na John Bocco walishindwa kuzitumia kwa nyakati tofauti.
Hata hivyo timu zote zilimaliza pambano zikiwa pungufu baada ya Mohamed Ibrahim naye kutolewa nje kwa kadi ya pili ya njano kufuatia kuadhibiwa kwa kosa la kumkanyaga Shomari Kapombe.
Kwa ushindi wa leo, Simba itamsubiri mshindi kati ya wenyeji Mbao na Yanga katika nusu fainali ya kesho itakaypigwa CCM Kirumba
Beki Mkongo, Janvier Besala Bokungu akaizuia Azam FC kusawazisha baada ya kuokoa mpira uliopigwa kwa kichwa na Nahodha wa timu hiyo, John Raphael Bocco uliokuwa unaelekea nyavuni dakika ya 84.
Kikosi cha Simba kilikuwa; Daniel Agyei, Janvier Bokungu, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murshid, James Kotei/Said Ndemla dk88, Jonas Mkude, Shizza Kichuya, Muzamil Yassin, Laudit Mavugo/Mwinyi Kazimoto dk86, Ibrahim Hajib na Mohammed Ibrahim.
Azam FC; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Gardiel Michael, Aggrey Morris, Daniel Amoah, Himid Mao, Stephan Kingue/Joseph Mahundi dk58, Shaaban Iddi/Frank Domayo dk46, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na Ramadhani Singano ‘Messi’/Mudathir Yahya dk82.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni