Kelvin Naftali alikua wa kwanza kuipatia Serengeti Boys bao kwa kichwa akimalizia krosi ya kona fupi iliyopigwa na Nickson Kababage dakika ya sita ya mchezo.
Angola waliweza kusawazisha dakika nane baadae kwa mpira wa kichwa kupitia kwa Pedro, baada ya krosi iliyopigwa upande wa kulia kuwazidi walinzi wa Serengeti pamoja na mlinda mlango Ramadhan Kabwili.
Mabadiliko ya benchi la ufundi kipindi yaliongeza uhai kwa Serengeti Boys na kujipatia bao la pili kupitia kwa mshambuliaji wake Abdul Suleiman aliyeitumia vyema nafasi ya Yohana Mkomola na kuukwamisha mpira wavuni.
Kwa matokeo ya leo, Serengeti Boys imefikisha pointi 4 ikiongoza msimamo wa Kundi B, ikifuatiwa na Niger, Mali na Angola zote zenye pointi moja, huku baadae kukiwa na mchezo kati ya Mali v Niger.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni