Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, kinatarajiwa kwenda Kigali, Rwanda kesho Jumatano mchana kikitokea Mwanza, Tanzania.
Taifa Stars iliyokuwa jijini Mwanza kwa kambi kabla ya kucheza mchezo wa
kwanza dhidi ya Rwanda Jumamosi iliyopita, itapitia Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere kwenda Rwanda.
Stars itaondoka Mwanza kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania majira
ya saa nne asubuhi na kuwasili Dar es Salaam majira ya saa sita mchana
kabla ya kuunganisha ndege ya Rwanda majira ya saa nane alasiri kwenda
Kigali, Rwanda.
Inakwenda Kigali kwa ajili ya mchezo wa marudiano na Rwanda maarufu kama
Amavubi kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa
wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN 2018). Fainali za CHAN mwakani
zitafanyika nchini Kenya.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza timu
hizo zilitoka sare ya bao 1-1. Mshindi wa jumla katika michezo miwili,
atakuwa amesonga mbele hivyo kukutana na Uganda mwezi ujao.
Katika mchezo huo wa marudiano utakachezwa Kigali Rwanda, Kocha Mkuu wa
Taifa Stars, Salum Mayanga atamkosa beki wake wa kulia, Shomari Kapombe
anayesumbuliwa na mguu alioumia katika mchezo kwanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni