SARE ya bao moja iliyoipata timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ dhidi ya Rwanda ‘Amavubi’ imeiweka kwenye mazingira magumu ya kufuzu fainali za michuano ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani (CHAN) 2018.
Stars iliyoshindwa kuutumia vema uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza itapaswa kushinda katika mchezo wa marudiano utakaofanyika jijini Kigali Julai 23 au kupata sare ya mavao kuanzia mawili ili kupata nafasi ya kufuzu kwa fainali hizo.
Amavubi walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 17 kupitia kwa Dominique Nshitu baada ya mabeki wa Stars kuzembea kuokoa mpira wa krosi iliyopigwa kutoka upande wa kulia.
Beki wa kulia wa Stars Shomari Kapombe alishindwa kuendelea na mchezo na kutolewa dakika ya 22 baada ya kuumizwa na mchezaji wa Rwanda nafasi yake ikachukuliwa na Boniface Maganga.
Mabishano yalitokea uwanjani dakika ya 51, baada ya beki Salim Mbonde wa Taifa Stars kuunawa mpira nje kidogo ya boksi wakati akiokoa, lakini wachezaji wa Rwanda wakasema aliunawia ndani.
Na refa Alier Michael James akatofautiana na msaidizi wake namba moja, Abdallah Suleiman Gassim, wote wa Sudan Kusini aliyedai awali kweli tukio hilo lilifanyika ndani ya boksi, kabla ya baadaye kukubali ilikuwa nje
Himid Mao aliisawazishia Stars bao hilo dakika ya 34 kwa mkwaju wa penati baada ya beki Rucogoza Aimambe wa Amavubi kuunawa mpira katika jitihada za kuzuia krosi ya Gadiel Michael.
Stars walijitahidi kufanya mashambulizi kadhaa langoni mwa Amavubi lakini walishindwa kupenya safu ya ulinzi iliyokuwa makini kuondoa hatari zote.
Mshindi wa jumla wa mchezo huo atakutana na timu ya Uganda ili kufuzu michuano hiyo.
Kikosi cha Tanzania kilikwa; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Gardiel Michael, Nurdin Chona, Salim Mbonde, Erasto Nyoni, Simon Msuva, Himid Mao, John Bocco/Stahmili Mbonde dk93, Muzamil Yassin na Shiza Kichuya.
Rwanda; Ndayishimiye Eric, Marcel Mubumbyi/Latif Bishira dk63, Bizimana Djihad, Dominique Savio Nshuti/Innocent Nshuti dk94, Emmanuel Imanishimwe, Iradukunda Eric, Manzi Thierry, Mico Juastin/Kayumba Soter dk81, Yannick Mukunzi, Nsabimane Aimable na Rucogoza Aimable.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Jumamosi, 15 Julai 2017
TAIFA STARS YANG'ANG'ANIWA KIRUMBA, YALAZIMISHWA SARE NA RWANDA 1-1
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni