Timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania Taifa Stars wameondoshwa katika Michuano ya Kufuzu kwa fainali za Mataifa afrika kwa Wachezaji wanaocheza ligi za Ndani Yaani CHAN baada ya kutoka Sare ya 0-0 dhidi ya Rwanda.
Tanzania ambao walikuwa wakihitaji ushindi wa Aina yoyote au Sare ya kuanzia Mabao mawili, wameshindwa kufunga Bao lolote katika mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Nyamirambo Mjini Kigali, Rwanda.
Tanzania Ndio walioanza kwa kasi wakicheza Pasi fupifupi na za haraka Huku Rwanda wakionekana wazi Kama Wameingia kulinda Sare yao waliyoipata Katika mchezo wa kwanza.
Katika dakika ya 10 Pasi ya Mzamiru Yassin ilimkuta John Bocco Adebayor ambaye alituliza kwenye Kifua na kugeukia Lango la Rwanda na kupiga shuti lisilokuwa na Macho na kumlenga Mlinda Mlango Ndayishimiye Eric ambaye alipangua na kuwa Kona butu.
Dakika ya 33 na 35 Tanzania walifanya mashambulizi mengine Hatari Lakini kukosa umakini kwa John Bocco na Uimara wa safu ya Ulinzi Ya Amavubi kukafanya matokeo kuwa 0-0.
Amavubi walitulia baada ya Shambulizi hilo na kupanga Tena mashambulizi ambayo dakika ya 41 nusura yawapatie bao Lakini Dominique Nshuti alikosa kuunganisha Mpira Wavuni uliopigwa na Muhire Kevin.
Tanzania wakajibu mapigo kwa shambulizi La kushtukiza ambalo lilimkuta Simon Msuva Lakini alipiga kashuti Mtoto ambacho kaliishia mikononi mwa Mlinda Mlango Ndayishimiye Eric.
Kipindi cha pili kilipoaanza Tanzania waliongeza kasi zaidi na kosakosa ziliendelea Kama kawaida Huku nao Rwanda kupitia kwa Bizimana Djihad walikosa mabao Mengi pia.
Kocha Salumu Mayanga alifanya mabadilko katika dakika ya 62 kwa kumtoa Raphael Daudi na kumuingiza Said Hamis Juma Ndemla ili kuongeza kasi zaidi na kumiliki eneo la kiungo.
Lakini pia dakika ya 67 alimtoa Simon Msuva na kumuingiza Kiungo mchezeshaji Joseph Petro Mahundi Na dakika ya 75 alimtoa John Raphael Bocco na kumuingiza Kelvin Sabato Kongwe.
Dakika ya 83 Mlinzi wa Taifa Stars Erasto Nyoni katika harakati za kuuokoa mpira langoni mwake alijichanganya na kunyang'anywa Mpira ambao ilimkuta Mukunzi Yannick na kupiga shuti lilitoka sentimita Chache langoni mwa Stars.
Hadi kipyenga cha mwamuzi Brian Miro kutoka Uganda kinapulizwa Rwanda Ambao ndio wenyeji wa mchezo huo Sifuri na Tanzania Sifuri.
Rwanda Vs Uganda.
Kwa Matokeo hayo Rwanda wanasonga mbele kwa bao la ugenini walilolipata Katika Sare ya Bao 1-1 Juma lililopita Jijini Mwanza katika mchezo wa awali, Huku Tanzania wakiaga Rasmi.
Rwanda watakutana na Uganda katika hatua inayofuata, ambao wao wametoa Sudan Kusini kwa Mabao 4-0 katika mchezo mwingine wa ukanda huu wa Afrika ya Mashariki uliopigwa Nchini Uganda.
Mara ya Mwisho Tanzania kushiriki Michuano hii ni Mwaka 2009 wakiishia katika Hatua ya Makundi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni