Shirikisho la Soka nchini ‘TFF’ Limemtangaza Ammy Conrad Ninje
kuwa Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’
inayokwenda nchini Kenya kushiriki Michuano ya nchi za Ukanda wa Afrika
Mashariki na Kati ‘CECAFA Challenge 2017’.
Ninje ambaye ni Mtanzania, amekuwa msaada kwa Vijana zaidi ya 90
katika Academy ya Hull City ya nchini Uingereza, na anatarajia kutangaza kikosi
kitachoshiriki Michuano hiyo ya CECAFA siku ya Kesho.
Akizungumza mara baada ya utambulisho huo Kocha Ninje ameishukuru
TFF kwa kumchagua kuwa kocha wa Kilimanjaro Stars na ameahidi ataisaidia timu
hiyo kufanya vizuri katika mashindano hayo.
-TFF wameamua kunipa majukumu ya kuifundisha Kilimanjaro Stars,
nipo tayari kwenda na kushinda mashindano hayo n tuhakikishe tunarudi hapa na
kombe, Amesema kocha Minje
Kundi A.
Tayari ratiba ya michuano hiyo imekwishatoka ambapo Kilimanjaro
Stars ambayo ipo kundi A pamoja na timu za Zanzibar, Kenya, Libya na Rwanda
watafungua dimba na Libya Disemba 3.
Mashindano hayo ya kila mwaka yanafanyika kwa mara ya kwanza toka
mwaka 2015 ambapo Uganda walifanikiwa kutawazwa Mabingwa, na mashindano ya
mwaka huu yanatarajiwa kufikia tamati Disemba 17, ambapo jumla ya timu 10
zimethibitisha kushiriki.
Kundi B linatimu za Burundi, Ethiopia, Sudani Kusini, Uganda
pamoja na timu mwalikwa Zimbabwe.
Ratiba ya CECAFA
Jumapili 3 Disemba: Libya v Tanzania [2PM]; Kenya v Rwanda [4PM]
Jumatatu 4 Disemba: Burundi v Ethiopia [2PM]; Uganda v Zimbabwe [4PM]
Jumanne 5 Disemba: Zanzibar v Rwanda [2PM]; Kenya v Libya [4PM]
Jumatano 6 Disemba: S.Sudan v Ethiopia [2PM]; Uganda v Burundi [4PM]
Alhamis 7 Disemba: Tanzania v Zanzibar [2PM]; Rwanda v Libya [4PM];
Ijumaa 8 Disemba: S.Sudan v Ethiopia [2Pm]; Zimbabwe Burundi
[4PM]
Jumamosi 9 Disemba: Rwanda v Tanzania -2PM]; Kenya v Tanzania
[4PM]
Jumapili 10 Disemba: S.Sudan v Burundi [2PM]; Ethiopia v
Uganda [4PM]
Jumatatu 11 Disemba: Libya v Zanzibar [2PM]; Kenya v Tanzania
[4PM]
Jumanne 12 Disemba: Uganda v S.Sudan [2PM]; Zimbabwe v
Ethiopia [4PM]
Jumatano: SIKU YA MAPUMZIKO
Alhamis: Disemba 14 1st semi-final - Mshindi Kundi B Vs
runners-up Kundi A
Ijumaa: Disemba 15 2nd semi-final -Mshindi Kundi B V
runners-up Kundi A
Jumamosi: Siku ya Mapumziko
Sunday 17 Disemba 17 : Mechi
ya Kutafuta Mshindi wa nafasi ya Tatu [2PM]
Final. [4PM]
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni