Ronaldo amefurahia kipindi cha miaka nane na nusu Bernabeu, akiwa ameshinda mataji mawili ya ligi na matatu Ligi ya Mabingwa miongoni mwa mafanikio yake, lakini ripoti zimedai kuwa supastaa huyo hana furaha na maisha ya Madrid.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 sasa imedaiwa kuwa hana mpango wa kusaini mkataba mpya kuendelea kuichezea miamba hiyo ya La Liga kwa mujibu wa Diario Gol, na jambo hilo limeishawishi PSG kuingia kwenye mbio za kuiwania saini yake.
Inasadikika mazungumzo yamefanyika hotelini Madrid, na wakala Jorge Mendes akisemekana kuwa tayari kushinikiza usajili huo ikiwa Ronaldo ataonyesha nia ya kuhamia Paris.
PSG walivunja rekodi ya uhamisho kwa kumsajili Nyemar kutoka Barcelona msimu uliopita wa majira ya joto, na miamba hao wa Ligue 1 watalazimika kuilipa Monaco fedha nono kumsajili Kylian Mbappe, lakini imedaiwa kuwa PSG wapo tayari kulipa kiasi chochote cha fedha kumsajili Ronaldo kikosini mwao.
Ronaldo amefunga goli moja tu katika mechi nane La Liga msimu huu, ingawa Mreno huyo amefunga mara nane Ligi ya Mabingwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni