Rais wa Real Madrid Florentino Perez ameweka tarehe ya mwisho majira ya joto 2018 kumsajili kipa wa Manchester United David De Gea, kwa mujibu wa Diario Gol .
Wakuu wa Barcelona wameungana kuhakikisha Philippe Coutinho anasaini mkataba kujiunga na klabu hiyo Januari, kwa mujibu wa Sport .
Mesut Ozil amependekezwa kuwa mbadala Barce ikiwa miamba hao wa Catalan watashindwa kuishawishi Liverpool kumuuza Coutinho dirisha dogo la uhamisho.
Lakini habari zimedai kuwa Coutinho bado anataka kuondoka Anfield, na kwamba ofa itakayofikia €150 milioni itatosha kuishawishi Liverpool kumuuza, na Liverpool haitaki kufikiria mchezaji mwingine tofauti.
ARSENAL KUMSAJILI FEKIR
Arsenal itafanya mpango wa kumsajili Nabil Fekir kutoka Lyon, kwa mujibu waTuttoMercatoWeb .
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 sasa amekuwa akifuatiliwa na Barcelona, Juventus na Atletico Madrid, lakini Gunners wanatumai kumsajili kuwa mshambuliaji wao.
Arsenal wanapewa nafasi kubwa kumsajili Jakub Jankto kutoka Udinese baada ya Juventus kuacha mpango wa kumsajili, kwa mujibu wa Calciomercato .
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21 amekuwa akifuatiliwa na klabu zote mbili, lakini miamba wa Serie A hawapo kutoa fedha nyingi kumsajili hivyo kuwaachia Gunners nafasi.
SANE KULAMBA DILI MPYA CITY
Manchester City watampa Leroy Sane mkataba mpya ambao utamwezesha kulipwa £80,000 kwa wiki, kwa mujibu wa The Sun .
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani amekuwa mtu muhimu kwenye kikosi cha Pep Guardiola tangu ajiunge na City akitokea Schalke na mshahara kwae utapandishwa sasa, lakini atalazimika kuwasubiri Kevin De Bruyne, David Silva na Fernandinho kusaini mataba mpya kwanza.
MADRID YAJIPANGA KUMSAJILI LUIZ
Real Madrid wanaangalia uwezekano wa kumsajili beki wa Chelsea dirisha la uhamisho wa Januari, kwa mujibu wa Daily Telegraph .
Luiz amekosa maelewano mazuri na meneja wa Blues Antonio Conte katika wiki za hivi karibuni, jambo linaloashiria anaweza kuwekwa sokoni majira ya baridi.
Madrid nao wanataka kuimarisha safu yao ya ulinzi baada ya mwanzo mbaya msimu huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni