Louis van Gaal amesema Manchester United
haina mvuto zaidi chini ya Jose Mourinho kuliko yeye alivyokuwa meneja.
United ya Mourinho ilifungwa
2-1 na mahasimu wao Manchester City kwenye Ligi Kuu Uingereza Jumapili, na
kuachwa pointi 11 na timu hiyo ya Pep Guardiola kileleni mwa msmimo wa ligi.
Mreno huyo amelalamikiwa
kutumia mbinu za kujihami kwenye mechi kubwa tangu alipochukua mikoba ya Van
Gaal Old Trafford 2016
Van Gaal pia alilaumiwa kwa
kucheza mfumo usio na mvuto katika kipindi ambacho alikuwa kocha wa United
lakini Mdachi huyo amesisitiza kuwa timu yake ya zamani imekuwa hovyo zaidi
chini ya Mourinho kuliko ilipokuwa chini yake.
Akiongea na Fox Sports
Netherlands, Van Gaal alisema: "Kama ukiniuliza niliifanyia nini United,
naweza kusema ulikuwa mwaka wangu mzuri mno, kulingana na mazingira niliyokuwa
nikikabiliana nayo kazini.
"Na sasa nikiitazama
United, naweza kusema Mourinho hakosolewi wakati soka lake halina mvuto
kabisa...
"Kile United inachofanya sasa ni
soka la kujihami. Mimi nilicheza soka la kushambulia. Kithibiti ni kwamba
wapinzani walikuwa wakipaki basi mara zote.
"Hawafanyi hivyo sasa
kwa sababu Jose Mourinho anacheza kwa kujihami."
Mourinho alifanya kazi kama
msaidizi wa Van Gaal Barcelona kutoka 1996 hadi 2000, Guardiola akiwa nahodha
wa klabu kipindi hicho.
Sasa Mourinho na Guardiola
wanaziongoza klabu za Manchester kama mameneja na Van Gaal amesisitiza kuwa
timu yake ilikuwa ikicheza vizuri zaidi ya mwenzake.
Aliongeza: "Ni bora
niiangalie City ikicheza kuliko United.
"Unahitaji ubora kwenye
kikosi ni wazi kwamba City ni kikosi bora."
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni