ARSENAL INATAKA KUMSAJILI DAVID LUIZ
Arsenal wameandaa kitita cha £30milioni kwa ajili ya beki wa Chelsea David Luiz, kwa mujibu wa habari kutoka Daily Express .
Luiz ameichezea Blues mechi nane tu msimu huu Ligi Kuu Uingereza, baada ya kushindwa kumshawishi Antonio Conte.
Inafahamika kuwa mahusiano yao hayajapona vizuri, na Arsene Wenger sasa anavutiwa kuipata saini ya Mbrazili huyo.
Imeripotiwa kuwa Luiz ni shabaha ya Jose Mourinho na Manchester United, kadhalika Juventus na Real Madrid.
DE BRUYNE MBIONI KUSAINI MKATABA MPYA CITY
Kevin De Bruyne anakaribia kusaini mkataba mpya wa muda mrefu Manchester City, kwa mujibu wa BBC .
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ameibukia kuwa mmoja wa viungo bora katika ulimwengu wa soka akiiwezesha timu ya Guardiola kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Uingereza kwa pengo la alama 11.
ARTETA APANGWA KUWA MRITHI WA WENGER
Mikel Arteta ndiye anayeweza kupewa mikoba ya Arsenal kumrithi Arsene Wenger, kwa mujibu wa Daily Telegraph .
The former Spain international is currently working at Manchester City under Pep Guardiola, but is held in high regard by the Gunners.
Wenger's current contract expires in 2019, and Arsenal are working up a shortlist of replacements, with Arteta near the top of the list
Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Hispania kwa sasa anafanya kazi Manchester City chini ya Pep Guardiola, lakini anapewa nafasi kubwa na Gunners.
Mkataba wa Wenger unafikia mwisho 2019 na Arsenal wameanza kuangalia makocha wanaoweza kuwa mbadala wake, Arteta akiwa wa kwanza kwenye orodha.
DORTMUND WANANAMTAKA MKHITARYAN WAO
Borussia Dortmund wanaendelea kuonyesha nia ya kumrejesha mshambuliaji wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan kwenye klabu yao, kwa mujibu wa The Independent .
Mkhitaryan aliondoka Dortmund kutua Old Trafford majira ya joto 2016, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Armenia ameshindwa kuleta ushawishi chini ya Jose Mourinho.
Bosi wa United hajakataa uwezekano wa kuuza wachezaji Januari, na kufuatia habari zilizojiri anaweza kumruhusu Mkhitaryan kurejea Bundesliga na kumruhusu Mourinho kumsajili Julian Weigl.
MAN UTD YATENGA £60M KUMSAJILI SANDRO
Manchester United wanajipanga kutoa kitita cha paundi milioni 60 kwa ajili ya beki wa Juventus Alex Sandro uhamisho wa Januari, kwa mujibu wa Daily Mirror .
Bosi wa United amekuwa akivutiwa na kazi ya Mbrazili huyo mara kadhaa kwani anataka kuimarisha zaidi safu yake ya mabeki Old Trafford.
ARSENAL KULIPA €48M KUMSAJILI LOZANO
Arsenal wapo tayari kutoa €48 milioni kwa ajili ya nyota wa PSV Hirving Lozano, kwa mujibu wa habari kutoka Mexico.
Lozano anacheza Eredivisie msimu wake wa kwanza na ameshafunga magoli 10 na kutoa pasi sita za magoli katika mechi 15 tu msimu huu, akizivutia Gunners na Everton.
DORTMUND YAKARIBIA KUMPATA ROMERO
Borussia Dortmund inakaribia kumsajili Maximiliano Romero kutoka Velez Sarsfield, Bild limeripoti.
Mshambuliaji huyo, 18, anaweza kugharimu takribani €12 milioni, na Dortmund wanaamini anaamini atakuwa mrithi sahihi kwa Pierre-Emerick Aubameyang.
WEST HAM WAMTENGEA DAU ARTER
West Ham wanataka kumsajili Harry Arter kutoka Bournemouth, kwa mujibu wa The Sun .
Bosi wa Wagonga nyundo David Moyes anataka kuimarisha safu yake ya kiungo na anaamini kuwa Arter, ambaye hajapata nafasi kikosi cha kwanza msimu huu ni suluhisho sahihi.
BARCA YAKARIBIA KUMSAJILI KINDA WA ZAMANI WA CITY
Barcelona wanakaribia kumsajili kinda nyota wa zamani wa Manchester City Jose Angel Pozo, kwa mujibu wa Onda Cero .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni