Kamati ya mashindano ya michuano ya Mapinduzi Cup imetoa ratiba mpya ambapo katika ratiba hiyo inaonesha kuwa Mabingwa watetezi timu ya soka ya Azam FC itaanza kampeni ya kutetea taji lake siku ya Jumapili Disemba 31 dhidi ya timu ya soka ya Mwenge.
Aidha mechi za ufunguzi wa michuano hiyo zinatarajiwa kufanyika Ijumaa, Disemba 29 kwa michezo miwili ambapo Mlandege watacheza na wawakilishi wa Zanzibar katika michuano ya klabu Bingwa Afrika maafande wa JKU.
Siku hiyo pia wawakilishi wa Zanzibar katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika Zimamoto FC watacheza na timu kongwe ya Taifa Jang’ombe mchezo ambao utaanza majira ya saa 2:15 usiku.
Kwa upande wa Timu pendwa Tanzania, Simba na Yanga wao wataanza kampeni ya michuano hiyo Januari 2, ambapo Simba wao watacheza na Mwenge ili hali Yanga ambao wapo kundi B wao watacheza na Mlandege.
Michuano hiyo ambayo inafanyika kwenye uwanja wa Amani uliopo mjini Unguja inatarajiwa kumalizika Januari 13 ambapo jumla ya timu 11 kutoka Tanzania Bara, Zanzibar na Uganda zinashiriki.
Ikumbukwe kuwa kundi A lina timu za URA ya Uganda, Jamhuri na Mwenge za Zanzibar pamojan na Azam na Simba za Tanzania Bara, kundi B lina timu za Zimamoto, Mlandege, JKU,na Taifa ya Jan’gombe Zanzibar huku Yanga na Singida United zikitoka Tanzania Bara.
Ratiba kamili
Dec 29, 2017 Friday
Mlandege vs JKU
Jamhuri vs Mwenge
Zimamoto vs Taifa ya Jan’gombe
Dec. 30, 2017 Saturday
Zimamoto vs JKU
Taifa ya Jan’gombe vs Mlandege
Dec. 31,2017 Sunday
Azam vs Mwenge Group A
Jamhuri vs URA
Jan. 1, 2018 Monday
Mlandege vs Zimamoto
JKU vs Taifa ya Jan’gombe
Jan. 2, 2018 Tuesday
Singida united vs Zimamoto
Simba vs Mwenge
Yanga vs Mlandege
Jan. 3, 2018 Wednesday
URA vs Mwenge
Azam vs Jamhuri
Taifa ya Jan’gombe vs Singida united
Jan. 4, 2018 Thursday
JKU vs Yanga
Simba vs Jamhuri
Jan. 5, 2018 Friday
Mlandege vs Singida united
URA vs Azam
Yanga vs Taifa ya Jan’gombe
Jan. 6, 2018 Saturday
JKU vs Singida united
Simba vs Azam
Jan. 7, 2018 Sunday
Zimamoto vs Yanga
Jan. 8, 2018 Monday
Simba vs URA
Yanga vs Singida united
Jan.10,2018 Wednesday
1st Semi Final (Winner Group A, Runners Up Group ) 10:30 jioni
2nd Semi Final(Winner Group B, Runners Up GroupA) 2:15 usiku
Jan. 13, 2018 Saturday
MAPINDUZI CUP FINAL 2018 8:00 pm (saa 2:00 usiku)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni