STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 22 Januari 2018

HII HAPA RATIBA YA RAUNDI YA MWISHO MZUNGUUKO WA KWANZA VPL, YANGA NA AZAM, SIMBA WAPO TAIFA

Mzunguko wa kwanza wa ligi kuu soka Tanzania unatarajiwa kuhitimishwa Kati ya Januari 26 na 28 mwaka huu ambapo ratiba inaonesha vilabu vya Ruvu Shooting, Mwadui, Azam FC, Stand United, Mbeya City, Kagera Sugar, Simba na Singida United vitacheza mechi zao nyumbani.
Tokeo la picha la vpl tanzania
Mechi za kwanza katika kuhitimisha mzunguko wa kwanza zitafanyika Ijumaa ya Januari 26 ambapo siku hiyo kutakuwa na michezo miwili.

Washika mkia katika ligi hiyo Ruvu Shooting watakuwa nyumbani katika uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani Pwani kuumana na Wabishi Mbao FC.

Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana katika uwanja huo Mbao ambao kipindi hicho ndicho ilikuwa imepanda daraja iliwatungua Ruvu shooting mabao 4-1, Lakini pia walipokutana Mwanza kwa mara nyingine Mbao akashinda 2-0.

Siku hiyo hiyo katika nyasi za uwanja wa Mwadui Complex kutakuwa na kipute si cha kitoto, pale Njombe Mji watakapokwaana na wenyeji Mwadui FC.

Timu zote mbili zimetoka katika michezo ya raundi ya 14 kwa sare ambapo Njombe Mji walitoka sare ya 0-0 na Mtibwa Sugar wakati Mwadui walilazimishwa sare ya 1-1 na Ndanda hivyo ushindi ni muhimu kwa timu zote.

Azam Vs Yanga
Jumamosi ya Januari 27 mabingwa watetezi Dar Young Africans itawabidi kwenda Chamazi kuumana na Azam katika mchezo mwingine muhimu wa ligi.

Yanga ambao wamepoteza mchezo mmoja msimu huu, wanaenda kukutana na timu ambayo mbali na kuwa ngumu kufungika lakini pia hawajawahi kupoteza mchezo wowote wa ligi msimu huu.

Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbao FC katika mchezo wa raundi ya 14 Stand United siku hiyo ya Jumamosi watajitupa uwanjani kuwakaribisha wanakuchele Ndanda FC.

Mchezo huo unatarajiwa kufanyika katika dimba la CCM Kambarage mjini Shinyanga na unatabiriwa kuwa mchezo mgumu kwani kila timu inasaka alama tatu zitakazowatoa mkiani.

MCC vs Mtibwa 
Jijini Mbeya, katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine wenyeji timu ya soka ya Mbeya City inayomilikiwa na halmashauri ya jiji watakuwa na kibarua kizito dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mbeya City itawabidi kujiuliza sana watakapokuwa wanajiandaa na mchezo huo kwani wamekuwa na matokeo yasiyo ya kuridhisha kwa siku za hivi karibuni na ushindi wowote inamaana utarejesha hali ya kujiamini kwa wachezaji na benchi la ufundi.

Wanankurukumbi, Kagera Sugar watakuwa katika uwanja wao wa nyumbani siku hiyo ya Jumamosi kucheza na Wanapaluhengo Lipuli FC.

Kocha wa Kagera Sugar Mecky Mexime ambaye alichaguliwa kuwa kocha bora msimu uliopita anatakiwa kurejesha imani kwa mashabiki wa timu hiyo baada ya kupoteza michezo miwili mfulululizo mpaka sasa kwenye ligi hiyo inayoingia duru la pili.

Simba Vs Majimaji. 
Januari 28 kutakuwa na michezo miwili ya kuhitimisha mzunguko wa kwanza kwa msimu wa 2017/2018.
Vinara Simba SC watawakaribisha Majimaji FC katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Simba itawabidi kufanya kazi ya ziada kwani tayari Majimaji wameonesha ushindani hasa baada ya kutoka sare mbili mfulululizo na vigogo vya soka nchini Azam FC na Singida United.

Lakini pia mchezo huo Majimaji itawabidi wauendee kwa tahadhali kubwa hiyo ni baada ya Simba kuwachapa Singida United kwa mabao 4-0 katika mchezo ambao ulikuwa ni kwanza kwa Simba kucheza kwenye uwanja wa Taifa.

Mzunguko wa kwanza utahitimishwa kwa mchezo nambari 120 ambapo Wajelajela Tanzania Prisons wamesafiri hadi mkoani Singida kucheza na Singida United katika uwanja wa Namfua mjini humo.

Simba bado vinara. 
Mpaka sasa Simba ndio vinara wakiwa na alama 32 wakifuatiwa kwa karibu na Azam FC wenye alama 30 wakati Yanga wao wapo nafasi ya tatu wakiwa na alama 25.

Wakati mkiani mwa msimamo wapo Kagera Sugar wenye alama 12 katika nafasi ya 14, Njombe Mji wao wanaalama 12 pia katika nafasi ya 15 na Ruvu Shooting ya Masau Bwire wanashika mkia wakiwa na alama 11.

Ikumbukwe msimu ni timu mbili ndizo ambazo zitashuka daraja ili kupisha timu sita kutoka ligi daraja la kwanza tayari kwa msimu wa 2018/2019.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox