Kamati ya Tuzo za VPL, imekamilisha orodha ya awali ya wachezaji 30 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msimu wa mwaka 2017/18, ambayo sherehe zake zitafanyika Juni 23 mwaka huu.
Kila mwezi Kamati ya Tuzo, imekuwa ikitangaza jina la mchezaji aliyefanya vizuri kwa mwezi husika kutokana na vigezo mbalimbali na pia ripoti kutoka kwa makocha waliopo katika viwanja ambavyo ligi hiyo inachezwa.
Wachezaji walioshinda tuzo za mwezi ligi ya msimu huu na miezi yao katika mabano nimshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi (Agosti), beki wa Singida United, Shafiq Batambuze (Septemba) na mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa (Oktoba). Wengine ni kiungo wa Singida United, Mudathir Yahya (Novemba), mshambuliaji wa Mbao FC ya Mwanza, Habibu Kiyombo (Desemba), mshambuliaji wa Simba, John Bocco(Januari), kiungo wa Yanga, Papy Tshishimbi (Februari), mshambuliaji wa Lipuli, Adam Salamba (Machi) na mshambuliaji wa Majimaji, Marcel Kaheza (Aprili).
Wachezaji hao kila mmoja amepewa zawadi ya tuzo, king'amuzi cha Azam na fedha taslimu sh. Mil. Moja kutoka kwa wadhamini Vodacom.
Hivyo wakati huu tukielekea mwisho wa ligi, leo tunatangaza wachezaji 30 ambao watawania tuzo hiyo, ambao watachujwa na kubaki 10, kisha watabaki watatu ambao ndiyo wataingia fainali ya kuwania tuzo siku ya mwisho.
Wachezaji hao 30 ni
1. Habibu Kyombo (Mbao)
2. Khamis Mcha- Ruvu Shooting
3. Yahya Zayd-Azam
4. Razack Abalora-Azam
5. Bruce Kangwa-Azam
6. Aggrey Morris -Azam
7. Himid Mao –Azam FC
8. Awesu Awesu –Mwadui
9. Adam Salamba-Lipuli
10. Mohammed Rashid-Prisons
11. Shafiq Batambuze-Singida
12. Mudathir Yahya-Singida United
13. Marcel Kaheza- Majimaji
14. Ditram Nchimbi-Njombe Mji
15. Eliud Ambokile- Mbeya City
16. Shaaban Nditi-Mtibwa
17. Tafadzwa Kutinyu-Singida
18. Ibrahim Ajibu- Yanga
19. Gadiel Michael-Yanga
20. Papy Tshishimbi-Yanga
21. Kelvin Yondani-Yanga
22. Obrey Chirwa-Yanga
23. Aishi Manula-Simba
24. Emmanuel Okwi-Simba
25. John Bocco-Simba
26. Jonas Mkude-Simba
27. Erasto Nyoni-Simba
28. Shiza Kichuya-Simba
29. Asante Kwasi –Simba
30. Hassan Dilunga-Mtibwa
Licha ya Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwaka wa ligi, pia kunatolewa tuzo mbalimbali, ambapo kwa mwaka huu tuzo moja imeondolewa na nyingine imeongezwa ikiwa ni katika kuboresha.
Tuzo iliyoondolewa ni ya Mchezaji Bora wa Kigeni na imefanyika hivyo ili kuwapa fursa wachezaji wote kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL badala yakuwatenganisha.
Pia msimu huu imongezwa Tuzo ya Mwamuzi Bora Msaidizi ambayo haikuwepo msimu uliopita, hiyo ni kutokana kuthamini nafasi ya waamuzi wasaidizi.
Kwa mazingira hayo tuzo zitakazotolewa Juni 23, ambapo wadhamini wakuu ni Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom ni hizi zifuatazo:
Bingwa
Mshindi wa Pili
Mshindi wa Tatu
Mshindi wa Nne
Mfungaji Bora
Timu yenye nidhamu
U20 Player (Tuzo ya Ismail Khalfan)
Mchezaji Bora Chipukizi
Mwamuzi Bora Msaidizi
Mwamuzi Bora
Kipa Bora
Kocha Bora
Goli Bora
VPL Best Eleven
Mchezaji wa heshima
Zawadi kwa kila kategori pamoja na majina ya wanaowania tuzo ukiacha bingwa, mshindi wa pili, wa tatu, wa nne na mfungaji bora ambao hujulikana kulingana na ligi inavyoendelea zitatangazwa siku za usoni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni