STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumapili, 5 Aprili 2015

NI YANGA NA WATUNISIA, TP MAZEMBE YAPENYA

Wawakilishi pekee wa Tanzania Yanga imefahamika sasa kukutana na Etoile du Sahel ya Tunisia baada ya waarabu hao kulazimisha sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Benfica de Luanda ya Angola katika mechi yao ya marudiano ya Kombe la Shirikisho.
Etoile imesonga mbele kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya mchezo wa kwanza nyumbani kushinda bao 1-0 na sasa watavaana na Yanga waliosonga mbele dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe ambao jana waliwacharaza bao 1-0.
Kipigo hicho cha ugenini hakikuizuia Yanga kusonga mbele kwani ilikuwa na hazina ya ushindi wa mabao 5-1 yaliyopatikana katika mechi ya kwanza jijini Dar es Salaam.
Mechi ya mkondo wa kwanza ya Yanga na Etoile itachezwa kati ya April 17-19 jijini Dar es salaam kabla ya kurudiana mjini Tunisia wiki mbili baadaye ambapo mshindi atasubiri kucheza mchujo wa mwisho dhidi ya timu zitakazoangukia pua kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baadaye Juni tayari kwa ajili ya kutinga hatua ya makundi kuvuna mamilioni ya CAF.
Aidha TP Mazembe ya DRC imesonga mbele kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuitoa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya leo kushinda nyumbani 3-1 na kulipa kisasi cha kufungwa bao 1-0 ugenini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox