MABAO
ya vichwa ya Wilfried Bony na Gervinho yaliyopishana kwa sekunde 98
yameipa mwanzo mzuri Ivory Coast katika Kombe la Dunia baada ya kuilaza
Japan 2-1 katika mchezo wa Kundi C mjini Recife, Brazil.
Tembo
hao wa Ivory Coast walimuanzishia benchi Nahodha wake, Didier Drogba
lakini ni kuingia kwake ndiko kulikuja sambamba na mabao hayo.
Nyota
wa Japan, Keisuke Honda aliifungia timu yake bao la kuongoza dakika ya
16 kabla ya Ivory Coast kusawazisha kupitiakwa Bony dakika ya 64 na
Gervinho kufunga la pili dakika ya 65. Mapema katika mchezo uliotangulia
jana wa kundi hilo Colombia iliiaza 3-1 Ugiriki.
Kikosi cha Ivory Coast kilikuwa: Barry, Aurier, Bamba, Zokora, Boka/Djakpa dk75, Tiote, Yaya Toure, Die/Drogba dk62, Gervinho, Bony/Konan dk77 na Kalou.
Japan: Kawashima, Uchida, Morishige, Yoshida, Nagatomo, Yamaguchi, Hasebe/Endo dk53, Okazaki, Honda, Kagawa/Kakitani dk86 na Osako/Okubo dk68.

Mwanzo mzuri: Mshambuliaji wa Ivory Coast, Gervinho akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao la ushindi alfajiri ya leo
Mkali wao: Keisuke Honda akiifungia bao la kuongoza Japan
Mchezaji bora: Mwanasoka Bora wa Afrika, Yaya Toure (katikati) akipambana na wachezaji wa Japan
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni