BUNGE LA TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA
WADAU KUTOA MAONI YA MISWADA YA SHERIA YA: VALUE ADDED TAX ACT, 2014, TAX ADMINISTRATION ACT, 2014 NA FINANCE ACT, 2014
_____________
Katibu wa Bunge anawatangazia
wananchi wote kwamba Kamati ya Bunge ya Bajeti itaanza kuchambua Miswada
ya Sheria ya: Value Added Tax Act, 2014, Tax Administration Act, 2014
na Finance Act, 2014 siku ya Jumanne tarehe 17 Juni, 2014 kwa lengo la
kuuboresha kabla ya kupelekwa Bungeni kusomwa mara ya pili na hatimaye
kutungwa kuwa Sheria.
Kwa mujibu wa Kanuni ya 84(2) ya
Kanuni za kudumu za Bunge, Toleo la April, 2013 Kamati ya Bunge
iliyopelekewa Muswada na Mheshimiwa Spika inaweza kumwalika mtu yeyote
au taasisi yoyote kwa njia ya matangazo au kwa kuwaandikia barua ya
mwaliko kufika mbele ya Kamati na kutoa maoni yao.
Hivyo basi, Kamati ya Bajeti
inakaribisha wadau wenye maoni ya kuboresha miswada ya Value Added Tax
Act, 2014, Tax Administration Act, 2014 kuwasilisha maoni hayo kwa
Maandishi kwa Katibu wa Bunge, Ofisi ya Bunge, S.L.P 941, Dodoma. Kikao
cha kusikiliza na kupokea maoni hayo kitafanyika siku ya Jumanne tarehe
17 na Jumatano tarehe 18 Juni, 2014.
Maoni kwa ajili ya Finance Act
yatapokelewa na kusikilizwa siku ya Alhamisi tarehe 19 na Ijumaa tarehe
20 Juni, 2014. Aidha, Kamati inapendekeza kuwa maoni yawasilishwe
kupitia makundi ama asasi zenye maslahi yanayofanana ili yaweze
kushughulikiwa kwa pamoja.
Maoni kuhusu Miswada hiyo,
yatasikilizwa katika tarehe tajwa kuanzia saa 5.00 asubuhi, Ukumbi wa
Msekwa uliopo Bungeni Dodoma. Aidha, maoni hayo yanaweza kutumwa kwa
njia ya barua pepe kwa anuani lkitosi@parliament.go.tz. Kwa ufafanuzi zaidi wasiliana na Sekretarieti ya Kamati kupitia nambari +255716909526, +255785570685 au +255756160006.
Miswada hiyo inapatikana katika Tovuti ya Bunge www.parliament.go.tz.
Imetolewa na:
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa
Ofisi ya Bunge
DODOMA
14 Juni 2014
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni