Mvulana mdogo aliyezaliwa na mkia unaofikia urefu wa inch saba
anatarajia kufanyiwa upasuaji ili utolewe licha ya kuwa anaabudiwa kama
Mungu na watu wa jamii yake.
Arshid Ali Khan, mwenye miaka 13 anaweza kuathiriwa ukuaji wake kutokana
na mkia huo ingawa unamfanya aonekana kama alama ya uponyaji katika
Jimbo la Punjab, India. Mtoto huyo anayetumia kiti cha watu wenye
ulemavu amekuwa akiabudiwa na watu wa jamii yake kama Mungu aliyepewa
jina la Balaji.
Khan anasema mkia huo amepewa na Mungu na anaabudiwa kwasababu ni Mungu
huyo huyo ndiye anayemuomba ambapo maombi ya watu hugeuka kuwa kweli.
Anasema hajisikii vizuri wala vibaya kuwa na mkia huo yeye anaona sawa
tu. Arshid sasa anaishi na babu yake Iqbal Qureshi, na wajomba zake
wawili baada ya baba yake kufariki akiwa na umri wa miaka sita na mama
yake kuolewa tena.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni