STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 9 Juni 2014

Rais Kikwete awaongoza maelfu kumlilia Mzee Small

Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Nyerere akiwa na Mkwere Original


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete leo amewaongoza maelfu ya waombolezaji waliojitokeza kumsindikiza kwenye makazi ya milele aliyekuwa mchekeshaji maarufu na mkongwe nchini, Said Ngamba 'Mzee Small'.
Rais Kikwete aliwaongoza waombolezaji hao waliojitokeza nyumbani kwa marehemu Mzee Small, Tabata Kisiwani jijini Dar es Salaam wakiwamo wasanii mbalimbali nyota na wanamuziki majira ya mchana wakati wa kisomo cha kumrehemu marehemu kabla mwili wake haujaenda kuzikwa jioni.
Rais Kikwete alipokewa kwenye msiba huo na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifamba na Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steven Nyerere na kupitiliza moja kwa moja hadi ndani kwenda kumpa pole mjane wa marehemu.

Baada ya robo saa alitoka na kwenda kuungana na waombolezaji wengine kwa kutia saini kitabu cha rambirambi kabla ya kuteta na mtoto wa marehemu Muhidini Said na kumkabidhi bahasha yenye risala yake na kisha kuondoka msibani hapo.
Mbali na Rais Kikwete, Rais wa TAFF na Mwenyekiti wa Bongo Movie, msiba huo ulihudhuriwa na nyota mbalimbali wa fani ya sanaa wakiwamo wacheza filamu kama JB, Richie, Dk Cheni, Shamsa Ford, Deoi Shija, Niva, Nova, Slim Omar, Mzee Chillo, Mzee Jangala, Sandra na wengine.
Miongoni mwa wanamuziki waliokuwepo kwenye msiba huo ni pamoja na Roman Mng'ande 'Romario' wa Msondo Ngoma, Cosmas Chidumule, Mafumu Bilal 'Bombenga' na waigizaji waliowahi kufanya kazi na marehemu enzi za uhai wake pamoja na Rais wa SHIWATA, Cassim Twalib 'Teacher'.
Baadhi ya wasanii akiwemo Steve Nyerere na Mzee Jangala waliuelezea msiba huo kuwa ni pigo kubwa siyo kwa familia ya marehemu bali wasanii wote kutokana na ukweli Mzee Small alikuwa mmoja wa waasisi wa michezo ya kwenye runinga na mkongwe aliyewasaidia vijana wengi akiwa kama mwalimu.
Pia walisema kifo cha Mzee Small umekuja kuwatonesha donda ambalo bado halijapona la kuondokewa na wasanii mfululizo ndani ya muda wa mwezi mmoja sasa.
Marehemu Mzee Small aliyezaliwa mwaka 1955 na kuanza sanaa mwaka 1980 ameacha mjane na watoto sita pamoja na wajukuu saba.
Mwisho

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox