STURRIDGE ANUSURIKA KUJERUHIWA NA KOPO LA HEINEKEN
Daniel Sturridge ndiye alipoteza nafasi muhimu
ya England kuifunga Honduras katika mechi yake ya mwisho ya kirafiki kabla ya
kwenda kuivaa Italia, Jumamosi ijayo.
Lakini naye akanusurika kujeruhiwa vibaya baada
ya shabiki kurusha kopo la bia aina ya Heineken ambalo lilimkosa sentimeta chache.
Kama lingempata, hakika mshambuliaji huyo wa
Liverpool angekuwa matatizoni na huenda angelazimika kupata matibabu
hispitalini.
Hata hivyo, haikujulikana shabiki yupi alirusha
kopo hilo kutoka jukwaani wakati England ikitika sare bila ya kufungana dhidi
ya Honduras mjini Miami, Marekani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni