STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 18 Julai 2014

AFCON 2015: UZOEFU WA MART NOOIJ MSUMBIJI KUIBEBA TAIFA STARS?

TFF-TANZANIA-MSUMBIJIWIKIENDI hii Afrika itashuhudia Mechi 7 za kwanza za kuwania kuingia Makundi 7 ya kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, huko Morocco Mwakani na Tanzania inaanza Nyumbani Jumapili kwa kucheza na Msumbiji.
Tanzania, maarufu kama Taifa Stars, wako chini ya Kocha Mart Nooij ambae kati ya Mwaka 2007 na 2011 alikuwa Kocha wa Msumbiji na hilo huenda likaisaidia sana Stars kuisoma vizuri Msumbiji.
Pia Kikosi cha Stars, ambacho kilikuwa Kambini huko Botswana kwa Wiki mbili na kisha kwenda Mbeya, kimeimarika kwa kuwapata
Maprofeshenali wake Watatu ambao ni Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta wa Klabu ya TP Mazembe ya Congo DR na Mwinyi Kazimoto anaechezea Klabu ya Al Markhiya ya Qatar.
Kwenye Raundi iliyopita, Taifa Stars iliibwaga Zimbabwe kwa Jumla ya Mabao 3-2 baada ya kushinda Mechi ya Kwanza Bao 1-0 Jijini Dar es Salaam na kutoka 2-2 huko Harare.
Mshindi wa Mechi kati ya Taifa Stars na Msumbiji ataingia Kundi F ambalo lina Timu za Zambia, Cape Verde na Niger.
Kwngineko, Uganda, ambao walikuwa wacheze na Equatorial Guinea, sasa wataivaa Mauritania baada ya Equatorial Guinea kutupwa nje na CAF.
Mauritania, ambao walitolewa na Equatorial Guinea, walikata Rufaa kwa CAF kufuatia Equatorial Guinea kumchezesha Thierry Fidieu Tazemeta ambae hakustahili kwa vile ni Raia wa Cameroon.
Kenya, ambao wataivaa Lesotho Ugenini, watawakosa Maprofeshenali wao Denis Oliech, anaecheza France, na Kipa Arnold Origi ambae yuko huko Norway, baada wote kunyimwa ruhusa na Klabu zao kwa vile Mechi hizi zipo nje ya Kalenda ya FIFA lakini Victor Wanyama wa Southampton atakuwepo huko Maseru baada ya Klabu yake kumruhusu.
Mechi za Marudiano zitachezwa Wikiendi ya Agosti 1 hadi 3.
AFCON 2015-MOROCCO
RATIBA
[Saa za Bongo]
Jumamosi Julai 19
16:00 Uganda v Mauritania
16:30 Botswana v Guinea-Bissau
19:30 Sierra Leone v Seychelles
Jumapili Julai 20
16:00 Lesotho v Kenya
16:00 Tanzania v Mozambique
17:30 Congo v Rwanda
18:00 Benin v Malawi
MAKUNDI:
KUNDI A
-Nigeria
-South Africa
-Sudan
-Mshindi Congo/Rwanda
KUNDI B
-Mali
-Algeria
-Ethiopia
Mshindi Benin/Malawi
KUNDI C
-Burkina Faso
-Angola
-Gabon
-Mshindi Lesotho/Kenya
KUNDI D
-Ivory Coast
-Cameroun
-Congo DR
-Mshindi Sierra Leone/Seychelles
KUNDI E
-Ghana
-Togo
-Guinea
Mshindi Uganda/Mauritania
KUNDI F
-Zambia
-Cape Verde
-Niger
-Mshindi Tanzania/Msumbiji
KUNDI G
-Tunisia
-Egypt
-Senegal
-Mshindi Botswana/Guinea-Bissau

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox