Bingwa: Mats Hummels alitoa mchango mkubwa Ujerumani kutwaa Kombe la Dunia, na sasa anataka kuhamishia mafanikio yake Man United
BEKI
Mats Hummels yuko mbioni kujiunga na Manchester United wiki hii
akitokea Borussia Dortmund kwa dau la Pauni Milioni 16, kwa mujibu wa
taarifa kutoka
Hispania.
Hispania.
Klabu
hizo mbili bado hazijafanya mazungumzo kwa ajili ya uhamisho huo,
lakini timu ya Old Trafford inajiamini mno inaweza kumpata beki huyo
hodari.
Mlinzi
huyo mwenye umri wa miaka 25 aling'ara kwenye Kombe la Dunia akiwa na
Ujerumani iliyoibuka bingwa nchini Brazil, kiasi cha kumvutia hadi kocha
mpya wa United, Louis van Gaal.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni