Furaha kuwa hapa: James Rodriguez akionyesha dole wakati anaingia kufanyiwa vipimo vya afya Real Madrid
MFUNGAJI bora wa Kombe la Dunia, James Rodriguez amefuzu vipimo vya afya kuelekea usajili wake wa Pauni Milioni 60 Real Madrid
Rodriguez
alitikisa kwenye Kombe la Dunia baada ya kutwaa Kiatu cha Dhahabu kwa
mabao yake sita akiwa na timu yake ya taifa, Colombia.
Na
sasa mchezaji huyo anakwenda kuungana na magalactico Cristiano Ronaldo
na Gareth Bale kuunda moja ya safu kali kabisa za ushambuliaji duniani
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni