Kadi ya uanachama ya Mohammed Bin Slum mbele na nyuma |
MGOGORO wa Coastal Union umechukua hatua mpya baada ya kiungo wa zamani wa klabu hiyo, Mohamed Bin Slum kuhamia kwa mahasimu, African Sports, pia ya Tanga.
Inafahamika familia ya Bin Slum ni Coastal damu, lakini baada ya mgogoro uliobuka baina ya familia hiyo na uongozi wa sasa wa klabu hiyo chini ya Mwenyekiti, Hemed Hilal ‘Aurora’- mpasuko umeibuka.
Bin Slum wamekuwa wakiisaidia Coastal kwa hali na mali chini ya uongozi wa Aurora, ikiwemo kusajili wachezaji na mambo mengine, lakini mwishoni mwa msimu, yakaibuka makubwa.
Uongozi
wa Coastal uliishutumu Bin Slum kujitangaza kupitia Coastal bila
malipo- na Mkurugenzi Mkuu wa familia hiyo, Nassor Bin Slum akaamua
kuachana na timu hiyo.
Lakini Nassor amesema atabaki kuwa mwanachama mwaminifu ndani ya timu hiyo, ingawa kwa kile kinachodhaniwa hasira dhidi ya uongozi wa Aurora, amehamishia mamilioni yake ya udhamini kwa timu za Stendi United ya Shinyanga, Ndanda ya Mtwara na Mbeya City ya Mbeya, zote za Ligi Kuu.
Mdogo wake, ambaye misimu miwili iliyopita aliichezea Coastal yeye hasira zake zimekwenda mbali zaidi kwa kuamua kabisa kuchukua kadi ya uanachama ya African Sports.
Kwa ujumla hamkani si shwari ndani ya Coastal Union kwa sasa, uongozi wa Aurora ukiwa unapingwa vikali na baadhi ya wanachama.
Wanachama wanataka kupanua wigo wa klabu kwa kuingiza wanachama wengi zaidi, lakini uongozi wa Aurora umegoma kutoa kadi mpya.
Wakati huo huo, habari zinavumishwa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya Habari kwa ujumla, kwamba uongozi wa Aurora tayari maji ya shingo baada ya Bin Slum kujitoa.
Na mchana wa leo zilichapishwa habari kwenye mitandao ya kijamii na ujumbe wa simu kusambazwa kwamba Aurora amejiuzulu, kabla ya Ofisa Habari wa klabu hiyo, Oscar Assenga kuibuka na kukanusha taarifa hizo.
Aurora na timu yake madarakani Coastal Union imetunisha kifua kuonyesha inaweza kuendesha timu bila fedha za Bin Slum kwa kusajili wachezaji wapya na kuwaongezea mikataba baadhi ya waliomaliza.
Lakini wachezaji wengi wapya waliosajiliwa hadi sasa ni kutoka timu zilizoshuka Daraja, mfano Ashanti United ambako imewachukua Hussein Swedi na Mnigeria Brighton Obinna.
Lakini akina Aurora wamemudu kumuongezea Mkataba kipa Shaaban Kado, ambaye huyo hawezi kuwa wa ‘bei rahisi’.

Mwana Kimanumanu; Mohammed Bin Slum sasa ni mwanachama wa African Sports |

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni