Fifa imetangaza
orodha ya majina 10 watakaowania tuzo ya mchezaji bora katika michuano ya Kombe
la Dunia - 2014 Golden Ball.
Wachezaji watatu
wametoka Argentina, Angel Di Maria, Javier Mascherano na Lionel Messi. Mahasimu
wao wa siku ya Jumapili Ujerumani, imetoa wachezaji wanne, Mats Hummels, Toni
Kroos, Phillip Lahm na Thomas Muller.
Wengine ni James
Rodriguez kutoka Colombia, Neymar wa Brazil na Arjen Robben wa Uholanzi.
Fifa pia imetangaza majina ya watakaowania tuzo ya golikipa
bora wa michuano hiyo. Keylor Navas wa Costa Rica, Manuel Neuer wa Ujerumani na
Sergio Romero wa Argentina watawania tuzo hiyo.
Wakati huohuo Memphis Depay wa Uholanzi, Paul Pogba
na Raphael Varane wa Ufaransa wamechaguliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora
chipukizi katika Kombe la Dunia.
Washindi watatangazwa baada ya mchezo wa fainali
siku ya Jumapili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni