Denti wa darasa la sita aliyenaswa kwenye kambi ya machangudoa akidaiwa kujihusisha na biashara haramu ya kuuza mwili
.
Fichua
Maovu (OFM) ya Global Publishers imemnasa denti wa darasa la sita
anayesoma shule ya msingi (jina linahifadhiwa kimaadili) kwenye kambi ya
machangudoa akidaiwa kujihusisha na biashara haramu ya kuuza mwili..
Tukio hilo lilijiri wiki iliyopita maeneo ya Kahumba mjini Morogoro usiku wa manane ambapo kachero wa OFM alipokea simu kutoka kwa watu walioumizwa na jambo hilo huku wakimwonea huruma kwani alikuwa akichukuliwa na mijibaba.
Mama
(Bi. Nasra Hamis) ambaye alikerwa na tabia ya mtoto wa umri huo
kujihusisha na biashara haramu ya kujiuza akiwa amesimama karibu naye.
OFM
ilipofika eneo la tukio ilimshuhudia binti huyo lakini ilipotaka kuita
polisi, wenzake waliokuwa wakijiuza naye walikuja juu wakitaka
kumshushia kipigo mwanahabari wetu.Kesho yake OFM ilikwenda kumsaka mtoto huyo ambapo mama aliyejitambulisha kwa jina la Nasra Hamis Ndehere alikuwa miongoni mwa wazazi waliojitokeza baada ya kukerwa na tabia ya mtoto huyo ya kujiuza.
Bi. Nasra Hamis akishiriana na OFM kusaidia zoezi la upatikanaji wa wazazi wa mtoto huyo kwa njia ya simu.
Baada
ya kumnasa, binti huyo alikiri kujihusisha na biashara hiyo haramu kwa
kisingizio cha ukali wa maisha baada ya kufiwa na wazazi wake, alidai
alikuwa akitafuta pesa ya kununulia nguo za Sikukuu ya Idd.
...Moja ya wanafunzi wenzake(kulia) aliyedai kuwa amekuwa akitega shule.
Pia
mtoto huyo alidai kuwa nyumbani kwao ni Mwanza na alipoulizwa kama
anaweza kuwasiliana na ndugu zake alijibu anaweza hivyo alipewa simu ili
awapigie lakini namba zao hazikuwa hewani.OFM kwa kushirikiana na mama huyo waliamua kumpeleka mtoto huyo Ustawi wa Jamii.
Umati ukishuhudia mkasa huo wa mwanafunzi wa darasa la sita wakati akihojiwa.
Katika
hali ya kushangaza, wakati wanaelekea Ustawi wa Jamii, walikutana na
msichana ambaye baada ya kuwaona alisema binti huyo siku hizi haonekani
shuleni kwani anasoma naye darasa moja.
Kufuatia kauli hiyo, mama huyo alimshushia kichapo kikali denti huyo hivyo kujaza umati.
Kufuatia kauli hiyo, mama huyo alimshushia kichapo kikali denti huyo hivyo kujaza umati.
..
Kachero anayeshirikiana na OFM akichukua maelezo kuhusu tukio hilo.
Baada
ya kuona hali hiyo, OFM ilijitosa kumnusuru denti huyo kwa kuita polisi
wa pikipiki ambao walifika fasta na kumpeleka mtoto huyo kituo kidogo
cha polisi Kata ya Mji Mpya mjini hapa ambapo alikabidhiwa kwenye Dawati
la Jinsia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni