Mtoto Devota Malole aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kilosa kufuatia mama yake kumtesa kwa kumfungia ndani na kumlaza chini kwa muda wa miaka mitano amehamishiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro baada ya afya yake kiafya kubadilika.
Mganga
mkuu wa hospitali ya wilaya ya kilosa Dr Shedrack Mponzi amesema
wamelazimika kumuhamishia mtoto huyo katika hospital ya rufaa ya mkoa wa
Morogoro baada ya hali yake kuwa mbaya na uchunguzi wa awali umebaini kuwa
anamagonjwa mbalimbali ikiwemo utapia mlo kwa kukosa lishe ambapo katika hospitali ya mkoa wa morogoro waandishiwetu wameshuhudia madaktari wakifanya kila juhudi za vipimo na matibabu.
anamagonjwa mbalimbali ikiwemo utapia mlo kwa kukosa lishe ambapo katika hospitali ya mkoa wa morogoro waandishiwetu wameshuhudia madaktari wakifanya kila juhudi za vipimo na matibabu.
Wasamaria
wema wamejitokeza katika hospitali ya mkoa wa Morogoro kumjulia hali
mtoto Devota ambapo mbunge wa jimbo la Morogoro Abdul Azizi Abood
amewataka maafisa ustawi wa jamii kuacha kulala na badala yake
watekeleze wajibu wao ipasavyo kuwasaidia watoto wanaoteseka nae
mfanyabiashara wa kampuni ya mabasi ya Alsaidi Omari Alsaidy ameahidi
kugharamia matibabu ya mtoto huyo hata kama italazimika kupelekwa nje ya
nchi kwa matibabu ili kunusuru maisha yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni