LOUIS van Gaal ameahidi kuwajumuisha Paul Scholes na Phil Neville katika benchi la ufundi la Manchester United.
Mholanzi huyo aliyeanza kazi rasmi United wiki hii amesema atawatafutia kazi ya kufanya katika benchi lake.
Ryan Goggs tayari alishateuliwa kuwa msaidizi wa pili wa Van Gaal na Nicky Butt alibaki kuwa kocha wa timu za vijana.
Kocha huyo wa zamani wa Uholanzi
amethibitisha kuwa Neville na Scholes ambao kwa pamoja walikuwa
wachezaji wa kikosi cha mwaka 1992 kilichoshinda kombe la FA, watapatiwa
kibarua cha kufanya.
Alisema: "Nicky Butt tayari anatusaidia. Tutatafuta kazi ya Paul Scholes na Phil Neville. Hicho ndicho tunataka".
"Tunatakiwa kurithi ubora wa watu hawa na tutazungumza na kila mtu binafsi na tusubiri na kuona"
Timu mpya: Van Gaal atasaidiwa na Ryan Giggs
Van Gaal akizungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza katika klabu ya Manchester United.
Neville aliletwa Old Trafford na kocha
aliyefukuzwa kazi, David Moyes kama msaidizi wake wa timu ya kwanza na
alibakishwa baada ya Giggs kuteuliwa kuiongoza Man United kwa muda
katika mechi nne za mwisho za msimu uliopita.
Inafahamika kuwa United walitaka
kumbakisha Neville kwa pointi kuwa mchezaji huyo wa kikosi cha 1992 ni
muhimu katika klabu hiyo, lakini kutokana na ujio wa Van Gaal majukumu
ya kocha huyo yanaweza kupunguzwa zaidi ukilinganisha na msimu uliopita.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni