Vidal,
mwenye Miaka 27 na Mchezaji wa Kimataifa wa Chile, ni mlengwa mkubwa wa
Meneja mpya wa Man United Louis van Gaal licha ya Klabu yake Mabingwa
wa Italy kusisitiza hauzwi.Lakini, kutokana na Juve kumuwania Fulbeki wa Man United, Patrice Evra, ambae mwenyewe Juzi aliuambia uongozi wa Old Trafford nia yake kuhamia Juve, inaelekea Dili ya Vidal itakuwa laini.
Imeripotiwa kuwa Man United wameongea na Wakala wa Vidal, Fernando Felicevich, alipokuwa huko England kukamilisha Uhamisho wa Mchezaji mwingne anaemwakilisha, Alexis Sanchez, ambae ameshatua Arsenal.
Ikiwa Vidal, ambae Juni Mwaka Jana alisaini Mkataba mpya na Juve, atahamia Man United huenda Mshahara wake kwa Wiki ukawa Pauni 230,000.
+++++++++++++++++++++++++++++++
MANCHESTER UNITED
NDANI
Ander Herrera (Athletic Bilbao) ADA HAIKUTAJWA
Luke Shaw (Southampton) ADA HAIKUTAJWA
NJE
Federico Macheda (Cardiff City) BURE
Jack Barmby (Leicester City) BURE
Rio Ferdinand AMEACHWA
Ryan Giggs AMEACHWA
Nemanja Vidic (Inter Milan) BURE
Alexander Buttner (Dynamo Moscow) ADA HAIKUTAJWA


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni