STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumapili, 27 Julai 2014

'MESSI, SUAREZ & NEYMAR WATAMALIZA WAPINZANI!'

KOCHA wa zamani wa Barcelona amedai kuongezwa kwa Straika wa Uruguay Luis Suarez kwenye Kikosi cha Barcelona kutawamaliza Wapinzani wao huko La Liga.
LUIS_ENRIQUEHenk ten Cate, aliekuwa Kocha Msaidizi chini ya Frank Rijkaard huko Nou Camp Miaka ya 2003 na 2008, amesema mashambulizi ya Mtu 3 ya Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar yatakuwa hatari na kusambaratisha Wapinzani.
Barca wamemsaini Luis Suarez mapema Mwezi huu kwa Dau la Euro Milioni 88 kutoka Liverpool na kuungana na Neymar, aliehamia hapo mwanzoni mwa Msimu uliopita, ili kuongeza nguvu wakijumuika na aliewahi kuwa Mchezaji Bora Duniani mara 4 Lionel Messi.
Ten Cate amesema Barca itakuwa ni tishio kubwa ikiwa tu Suarez ataelewana vizuri na kupatana na Messi na Neymar.
Amesema: “Messi, Suarez na Neymar ni wachezaji wazuri sana. Ni Mastaa na wanaweza kubadilisha Gemu Sekunde yeyote ile! Ni Wachezaji bora wenye sifa kubwa. Kitu muhimu ni wao kuelewana!”
Msimu uliopita Barca walitwaa Supercopa de Espana tu huku Mahasimu wao wakubwa Real Madrid wakitwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI, ikiwa ni mara yao ya 10, na Copa del Rey wakati Atletico Madrid wakitwaa Ubingwa wa La Liga.
Msimu ujao wa La Liga unaoanza Agosti 23 Barca watakuwa chini ya Kocha mpya Luis Enrique, aliewahi kuichezea Klabu hiyo na pia kuwa Kocha wa Barca B, na Ten Cate amewataka Mashabiki kumuunga mkono Kocha huyo mpya kwani ana
uhakika ataleta mafanikio.
Ameeleza: “Luis Enrique anahitaji muda na nina matumaini atapewa muda huo kwa sababu nahisi atafanikiwa. Ni Kocha imara mwenye ari kubwa!”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox