Kipa mpya: David Ospina aliisaidia Colombia kufika Robo Fainali katika Kombe la Dunia kabla ya kutolewa na Brazil
KLABU
ya Arsenal imekamilisha usajili wa kipa wa Nice, David Ospina kwa dau
la Pauni Milioni 3.2, kwa mujibu wa kocha wa klabu hiyo ya Ufaransa,
Claude Puel.
Ospina
aliivutia The Gunners kufuatia kuranya vizuri akiidakia Colombia katika
Kombe la Dunia hadi kuifikisha Robo Fainali, ambako walitolewa na
wenyeji, Brazil.
Mlinda mango
huyo mwenye umri wa miaka 25 anajiunga na timu hiyo ya Kaskaizni mwa
London kwa mkataba wa miaka minne. Puel amezungumzia habari za kuondoka
kwa Ospina alipohojiwa na Sky Sports na kusema: "Imethibitishwa, ndiyo.
Akiwa na umri wa miaka 25 ni muhimu kwake kupata uzoefu wa mashindano
mengine, hivyo ni uhamisho mzuri wake,".
Uwezo utamuweka mtu langoni: David Ospina (kushoto) atagombea mamba na kipa wa sasa wa kwanza wa Arsenal, Wojciech Szczesny
Inafahamika
kwa sasa kipa huyo anakwenda kuchukua nafasi ya Lukasz Fabianski,
ambaye amejiunga na Swansea, kwenda kuwa wa pili nyuma ya kipa namba
moja wa sasa wa klabu hiyo, Wojciech Szczesny.
Pamoja
na hayo, kocha Arsene Wenger amesema uwezo ndio utakaomfanya mmoja wao
awe kipa mamba moja wa klabu, huku Ospina akionekana kabisa kuitaka kuwa
chaguo la kwanza.
"Unajua
mwanzoni Szczensy atakuwa mamba moja, kisha tena uwezo wa mtu ndiyo
utaamua, ikiwa Ospina ataonyesha ni bora, atacheza,"aliiambia ESPN.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni