KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho
amethibitisha kuwa mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo, Didier Drogba anarudi
darajani
.
.
Nyota huyo raia Ivory Coast
aliitumikia Chelsea kwa miaka 8 na kuondoka mwaka 2012 ambapo
alijiunga Galatasaray ya Uturuki baada ya kutwaa kombe la UEFA
dhidi ya Bayern Munich.
Ingawa ana miaka 36 kwasasa,
Mourinho anaamini bado anaweza wa kucheza ligi kuu nchini England na michuano
ya kimataifa.
“Tunalifikiria hilo,” Mreno huyo
aliwaambia waandishi wa habari baada ya kuulizwa uwezekano wa Drogba kurudi.
“Tunahitaji kushinda mechi na
kushinda makombe na Didier ni moja ya washambuliaji bora barani Ulaya,”.
“Bado anao uwezo wa kucheza ligi
kuu na tunalifikiria sana hilo na hatuendeshwi kwa hisia”.
“Kama unamrudisha, si kwasababu
yeye ni Didier au alifunga magoli mengi muhimu katika historia yake Chelsea, au
kwasababu nahitaji msaidizi, hapana, namrudisha na maamuzi yamekuja mapema
kwasbaabu yeye kama mchezaji anaweza kuifanya timu kuwa imara”.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni