Hawatoki: Juventus ipo makini kuwabakisha wachezaji wake muhimu ikiwa ni pamoja na kiungo wake, Arturo Vidal (kushoto).
Vidal amekuwa akihusishwa kuondoka
Turini majira haya ya kiangazi, ambapo klabu za Man United na Real
Madrid zikitajwa kuiwania saini yake.
Lakini alipoulizwa kuhusu hatima yake, Vidal alisema: "Siendi Manchester".
Vidal aliwasili Italia baada ya likizo
na alipoulizwa na waandishi wa habari kama atabaki Juventus alisema:
"Siendi Manchester. Naweza kusema nitabakia Juve? Sijui.
"Nitazungumza na Allegri jumatatu na
tutaona. Sijazungumza na Allegri au mchezaji mwenzangu yeyote yule,
lakini siendi Manchester.
Gazeti la Italia la Gazzetta Dello Sport
pia liliripoti kuwa Juventus hawataki kumuuza kiungo huyo aliyebakisha
miaka mitatu katika mkataba wake-lakini wanaweza kushawishika na dau la
Euro milioni 45 (Paundi milioni 36).
Kwenye rada: Nyota wa kimataifa wa Chile, Vidal kwa muda mrefu anawindwa na Louis van Gaal
Maisha mapya: Manchester United wana matumaini ya kujijenga upya chini ya Louis van Gaal.
Gazeti hilo pia liliripoti kuwa Liverpool na Asernal zinaitaka saini ya Vidal.
Taarifa za Vidal kukataa kujiunga na Man
United zitamkata maini bosi wa timu hiyo ambaye kwa muda mredu
anamhitaji ili kuimarisha safu ya kiungo, licha ya kumsajili Ander
Herrera kutokea Atletico Madrid.
Vidal alijiunga na Juve mwaka 20011
akitokea Bayer Leverkusen na amefunga mabao 11 katika mechi 32
alizocheza na kuisaidia miamba hiyo ya Turini kutwaa ubingwa wa tatu
mfululizo msimu uliopita.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni