STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 25 Julai 2014

NAHODHA WA `BLACK STARS` ASAMOAH GYAN AJITIA KITANZI KINGINE AL AIN

Asamoah Gyan extends Al Ain contract
NAHODHA wa timu ya Taifa ya Ghana, ‘Black Stars’, Asamoah Gyan ameongeza  mkataba na klabu yake ya Al Ain mpaka mwaka 2018, klabu imetangaza kwenye tovuti yake rasmi.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Sunderland alibakisha miaka miwili katika mkataba wake wa miaka minne, lakini nyota huyo mwenye miaka 28 ameongeza mkataba jana alhamisi.
Gyan kwasasa amefikisha magoli sita katika kombe la dunia baada ya kufunga nchini Brazil na kuwa mchezaji wa Afrika  aliyefunga magoli mengi zaidi ukanda huu .
Kitendo cha kuongeza mkataba na klabu hiyo ya Garden City, Gyan amejisikia furaha na kuelekeza nguvu zote huko.
“Nimefurahi sana kuongeza mkataba wangu mpaka 2018 , naishukuru bodi ya klabu, uongozi na mashabiki wote kwa kuniunga mkono,” Gyan aliiambia Tovuti ya klabu.
“Nimekuwa na furaha tangu nilipowasili 2011, nina matumaini ya kuisaidia klabu kushinda makombe”.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana, ambaye awali alijiunga na klabu hiyo kwa mkopo mwaka 2011, amefunga magoli 82 katika mechi 66 za ligi alizocheza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox