MABINGWA wa England Manchester City wamedaiwa kutoa Mkanda wa Video
ukionyesha Beki wa FC Porto Eliaquim Mangala akisaini kujiunga na Klabu
hiyo.
Mangala, Beki wa France mwenye Miaka 23, amekuwa akihusishwa na City kwa muda mrefu katika kipindi hiki cha Uhamisho na aliwahi kuonekana Jijini Manchester lakini hakuna tamko rasmi ambalo limetolewa hadi sasa.
Hata hivyo, Mkanda wa Video kwenye Tovuti ya Man City ulimuonyesha Mchezaji huyo akitua Jijini Manchester na Ndege maalum na kupokewa rasmi na kisha kupimwa afya yake.
Lakini Man City imekanusha Video hiyo na kudai Tovuti yao iliingiliwa na ‘Wavamizi’ na kuweka taarifa ambazo si za kwao.
Mangala alikuwemo kwenye Kikosi cha France huko Brazil kwa ajili ya Kombe la Dunia lakini hakucheza hata Mechi moja.
Man City
Ratiba/Matokeo Mechi za Kujipima Kabla Msimu mpya:
13 Julai Dundee 2-0 Man City
18 Julai Heart of Midlothian 1-2 Man City (Sinclair, Kolarov)
23 Julai Sporting Kansas 1 Man City 4, Kansas, USA
Guinness International Champions Cup
27 Julai AC Milan v Man City, Heinz Field, USA
30 Julai Liverpool v Man City, New York, USA
2 Agosti Olympiacos v Man City, Bank Stadium, USA
Ngao ya Jamii
10 Agosti Man City v Arsenal, 17.00, Wembley Stadium

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni