Heshima: Kinda Raul de Tomas (kushoto) akimpongeza Bale baada ya kuifungia Real bao la kwanza katika mechi za kujiandaa na msimu
REAL
Madrid imefungwa kwa penalti 3-2 na Inter Milan katika michuano ya
Kombe la Kimataifa jana, kufuatia sare ya 1-1 mjini California,
Marekani.
Nyota wa Wales, Gareth Bale alitangulia kuifungia Real Madrid dakika ya 10 kabla ya Samir Handanovic kuisawazishia Inter Uwanja wa California Memorial.
Katika
mikwaju ya penalti, wachezaji wawili wa Real, Isco na Asier
Illarramendi mikwaju yao iliokolewa na kipa Juan Pablo Carrizo kabla ya
kinda Omar Mascarell kupaisha.
Inter itakutana na Manchester United mjini Washington Jumanne, wakati Madrid itamenyana na Roma mjini Dallas siku hiyo hiyo.
Shujaa: Kipa Juan Pablo Carrizo (katikati) akipongezwa na wenzake baada ya kuokoa penalti mbili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni