STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 26 Julai 2014

SELEMANI ABDALLAH MBAROUK AKARIBISHWA YANGA SC


KOCHA wa Yanga Marcio Maximo jana  amemkaribisha mshambuliaji wa  Coventry City  inayoshiriki ligi daraja la kwanza chini Uingereza Selemani Abdallah Mbarouk, kufanya mazoezi  na timu hiyo na endapo atamvutia aweze kumsajili kwa ajili ya kukitumikia kikosi chake msimu unaokuja
Mbaruku mwenye asili ya Zanzibar, ameiambia Goal ameichezea kwa kipindi cha misimu tisa timu hiyo ya Coventry City,na kupata uzoefu wa kutosha kuweza kuitumikia Yanga endapo Maximo ataridhishwa na kiwango chake.
“Wakala wangu Salimu ambaye nimekuwa naye tangu nipo kituo cha kukuza vipaji cha Afri Soccer cha Zanzibar ndiyo amenileta hapa Yanga ameniambia ni timu nzuri ambayo inaweza kunifikisha kule ambapo ninapataka”alisema Mbarouk.
Mbarouk aliyewahi kupitia Academy ya Chalsea ya Uingereza akiwa na miaka saba alisema alisifu mazoezi ya Maximo na uwezo wa wachezaji wa Yanga na kusema anahitaji kujifua zaidi ili aweze kuendana na kasi yao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox