STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 26 Julai 2014

INTERNATIONAL CHAMPIONS CUP YAANZA, LEO MAN UNITED v AS ROMA!

Mashindano makubwa ya Guinnes International Champions Cup yameanza Jana Usiku kwa Olympiacos kuichapa AC Milan Bao 3-0 na Leo Usiku Manchester United watacheza na AS Roma ya Italy.
ICC-2014Kwenye Mechi ya Kundi B Olympiacos iliichapa AC Milan ya Italy Bao 3-0 na Bao zao zilifungwa na Alejandro Dominguez, Anastasios Papazoglou na Andreas Bouchalakis.
Mashindano haya yanashirikisha Timu 8 zilizogawanywa Makudi mawili na Mshindi wa kila Kundi ndie anaingia Fainali hapo Agosti 4.
MAN UNITED v AS ROMA
Leo huko Sports Authority Field, Denver, Manchester United itaivaa AS Roma katika Mechi yao ya kwanza ya Kundi A.
Timu hizi zimewahi kupambana mara kadhaa lakini Mechi itakayokumbukwa na wengi ni ile ya Marudiano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ya Aprili 2007 iliyochezwa Old Trafford.
AS Roma walitinga kwenye Mechi hiyo wakiwa wameshinda Mechi ya kwanza Bao 2-1 lakini walichokikuta huko Old Trafford hawatakisahau maisha baada ya kutandikwa Bao 7-1.
AS Roma wanaoongozwa na Kocha Rudi Garcia na Uwanjani wanae Mkongwe Francesco Totti.
Pia AS Roma wanaweza kumchezesha Mchezaji wao mpya Ashley Cole aliesainiwa kama Mchezaji huru baada ya kumaliza Mkataba wake na Chelsea.
Man United, chini ya Meneja mpya Louis van Gaal, wanaingia kwenye Mechi hii wakitoka kwenye ushindi mkubwa walipoichapa LA Galaxy Bao 7-0 Majuzi huko Rose Bowl, Pasadena na kutwaa Chevrolet Cup.
VIKOSI VINATARAJIWA:
MAN UNITED [Mfumo: 3-5-2]:
De Gea,
-Smalling, Jones, Evans
;
-Valencia, Shaw, Fletcher, Cleverley; Mata;
-Rooney, Welbeck.
AS ROMA [Mfumo: 4-3-3]:
Skorupski;
-Somma, Benatia, Castan, Cole;
-Keita, Florenzi, Nainggolan;
-Totti, Iturbe, Ljajic
International Champions Cup
MAKUNDI
KUNDI A:
-Manchester United
-AS Roma
-Real Madrid
-Inter Milan
KUNDI B
-AC Milan
-Olympiacos
-Manchester City
-Liverpool
RATIBA
**Saa zikitajwa ni za Bongo
Ijumaa Julai 25
Olympiacos CFP 3 AC Milan 0
Jumamosi Julai 26
23:10 Manchester United v AS Roma
Jumapili Julai 27
1:00   Real Madrid CF v Inter Milan
23:00 AC Milan v Manchester City
Jumatatu Julai 28
02:00 Liverpool - England v Olympiacos CFP
Jumatano Julai 30
02:00 Manchester United v Inter Milan
05:15 Real Madrid CF v AS Roma
Alhamisi  Julai 31
02:00 Manchester City v Liverpool
Jumamosi Agosti 2
20:00 Inter Milan v AS Roma
22:00 Olympiacos CFP v Manchester City
23:06 Manchester United v Real Madrid CF
Jumapili Agosti 3
01:30 Liverpool v AC Milan
FAINALI
Jumatatu Agosti 4
Mshindi Kundi A v Mshindi Kundi B

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox