STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 26 Julai 2014

CAZORLA: "TUTAWAIGA ATLÉTICO KUTWAA UBINGWA!"

Kwenye Mahojiano rasmi na Gazeti maarufu la michezo huko Spain MARCA, Kiungo wa Arsenal Santi Cazorla amesema wao inabidi wawaige Atletico Madrid ili kutwaa Ubingwa England kwa mara ya kwanza tangu Msimu wa 2003/04.
SANTI-CAZORLACazorla, ambae ni Mchezaji kutoka Spain, amesema: “Nina matumaini makubwa. Kwa kuwasaini Alexis Sánchez na Mathieu Debuchy Klabu imeonyesha nia yake kujenga Timu ili kutwaa Ubingwa. Msimu huu tuna matumaini ya kutwaa Taji!”
Aliongeza: “Kwa kutwaa FA CUP tulijiondolea presha tuliyokuwa nayo ya kutotwaa Kombe. Msimu uliopita hatukuwa na Kikosi kikubwa na tuliathirika kwa majeruhi wengi pamoja na Theo Walcott, Aaron Ramsey, Jack Wilshere, Mikel Arteta na Lukas Podolski na hata mimi nilisumbuliwa sana na enka. Hilo lilitufanya tushindwe kuwakamata Chelsea, Manchester City na Liverpool.”
Mchezaji huyo wa zamani wa Málaga na Villarreal amesema mbio za Ubingwa za Msimu huu ziko wazi na ametamka: “City ni Mabingwa Watetezi, Man United wanajiimarisha sana na kwa sababu hawako Mechi za Ulaya mkazo mkubwa kwao utakuwa kwenye Ligi. Chelsea wamefanya usajili mkubwa kwa kuwachukua Diego Costa, Cesc Fàbregas, Didier Drobga na kurudi kwa Kipa Thibaut Courtois na Liverpool watabaki wapizani!”.
Cazorla alisema: “Atletico Madrid ni
mfano mzuri kuiga. Walikuwa na Msimu mzuri. Watu wengi hawaoni mafanikio yao na kuwapongeza kwa kutokujua kwamba ni ngumu mno kutwaa Ubingwa wa La Liga mbele ya Barca na Real Madrid!”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox