Gerrard, mwenye Miaka 34 na ambae alianza kuichezea England Mwaka 2000 kwenye Mechi waliyoifunga Ukraine 2-0, aliichezea England kwa mara ya mwisho huko Brazil Mwezi uliopita walipotoka Sare 0-0 na Costa Rica kwenye Mechi ya Kundi D la Fainali za Kombe la Dunia.
Akitangaza habari hizi, Gerrard alisema: “Nilisikia raha muda wote niliochezea Nchi yangu. Hii ni Siku ya huzuni kwangu.”
Kwenye Mechi hizo 114 alizocheza alifunga Bao 21 na kushiriki Mashindano makubwa 6.
Gerrard ataendelea kuichezea Klabu yake Liverpool ambayo alicheza nao Mechi yake ya kwanza kabisa Mwaka
1998 dhidi ya Blackburn Rovers.
Gerrard, ambae amekuwa Nahodha wa England mara 38, ndie Mchezaji wa 3 kwa kuichezea England mara nyingi akiwa nyuma ya Kipa Peter Shilton, Mechi 125, na David Beckham, Mechi 115.
Gerrard ametoa shukrani zake kwa wote aliokuwa nao wakati aliichezea England.
Nae Mwenyekiti wa FA, Chama cha Soka England, Greg Dyke, amemsifia Gerrard na kumwita ni Nguli wa kweli wa England.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni