Nahodha wa Uholanzi, Robin van Persie akishangilia na mchezaji mwenzake, Dirk Kuyt (juu) baada ya kuifungia timu yake bao la kuongoza kwa penalti katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu Kombe la Dunia dhidi ya wenyeji, nchini Brazil. Uholanzi ilishinda 3-0, mabao yake mengine yakifungwa na Daley Blind na Georginio Wijnaldum. Uholanzi inaondoka na rekodi ya kutofungwa katika fainali za mwaka huu, ikishinda mechi zote na kutoa sare mbili, moja ya Robo Fainali waliyofuzu kwa matuta na nyingine ya Nusu Fainali waliyotolewa kwa matuta na Argentina. Fainali ni usiku wa Jumapili kati ya Ujerumani na Argentina.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni