STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 22 Julai 2014

USAJILI LIGI KUU TFF YAONGEZA WIKI MBILI TIMU KUMALIZA MAMBO

TFF imesogeza mbele muda wa usajili kwa wiki mbili

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeongeza muda wa usajili kwa wiki mbili ili kuzipa klabu nafasi ya kukamilisha taratibu zinazotakiwa. Hivyo hatua ya kwanza ya usajili inakamilika Agosti17 mwaka huu badala ya
Agosti 3 ya awali.
Kutokana na marekebisho hayo, kipindi cha uhamisho kinakamilika Agosti 17 mwaka huu wakati pingamizi itakuwa kati ya Agosti 19 hadi 26 mwaka huu.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itathibitisha usajili kati ya Septemba 1 na 2 mwaka huu
Uhamisho wa kimataifa, usajili wa wachezaji huru, na utatuzi wa dosari za usajili unatakiwa uwe umekamilika kufikia Septemba 7 mwaka huu. Uthibitisho wa hatua ya mwisho ya usajili utafanywa Septemba 15 mwaka huu.
Kwa upande wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2014/2015 itaanza Septemba 20 mwaka huu, na ratiba itatolewa mwezi mmoja kabla ya kuanza ligi hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox