Mashambulizi: Waandamanaji walivamia uwanja na kuanzisha dhoruba ya kuwashambulia wachezaji wa Maccabi Haifa
MECHI kati ya timu Israeli ya Maccabi
dhidi ya Lille ya Ufaransa iliahirishwa baada ya waandamanaji wanaoiunga
mkono Palestina kuvamiwa uwanja.
Waandamanaji hao walioripotiwa kuwa na
asili ya Uturuki waliingia katika uwanja wa Austrian ambapo mchezo
ulikuwa unaendelea na kuwavamia wachezaji wa Maccabi na kuzua vurugu.
Mmoja wa wachezaji alionekana akizozana na shabiki kabla ya kuanza kurushiana makonde mazito.
Hata hivyo wachezaji wa Maccabi walifanikiwa kutoka uwanjani bila kujeruhiwa.
Tukio hili limekuja wakati huu ambao majeshi ya Israel yamevamia na kufanya uhalifu dhidi ya majeshi ya Hamas huko Gaza.
Hatari sana: Waandamanaji waliwavamiwa wachezaji wa Maccabi Haifa na kusababisha mechi kuahirishwa.
Waandamanaji wakizipiga ngumi na wachezaji wa Maccabi Haifa
Jamaa akaamua kumrudishia: Wachezaji wengi wa Maccabi Haifa walianza kuzipiga baada ya kuvamiwa
Kula buti kwanza kijana!: Waandamanaji wanaoiunga mkono Palestina waliwavamiwa wachezaji wa Maccabi Haifa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni