BEKI wa Napoli na Colombia Juan Camilo Zuniga aliemuumiza Neymar na
kumfanya ashindwe kuendelea kuchezea Nchi yake Brazil kwenye Fainali za
Kombe la Dunia amelazimika kupewa ulinzi mkali baada ya kupokea vitisho
kwa maisha yake.
Zuniga alimvaa Neymar wakati wa Mechi ya Robo Fainali ya Kombe la Dunia kati ya Brazil na Colombia na Goti lake kumpiga Neymar mgongoni na kumvunja Mfupa mdogo wa Mgongo.
Camilo Zuniga, Baba wa Mchezaji huyo, ameeleza masikitiko yake: “Baada Colombia kucheza na Brazil huko Maracana kwenye Mechi za Mchujo za Kombe la Dunia la Mwaka 2010, mwanangu aliniambia Siku moja anataka kucheza Ligi ya Brazil! Lakini sasa kwa usalama wake na Familia, hili halitawezekana!”
Mzazi huyo amesema wamekuwa wakipokea vitisho kwa maisha ya Juan Camilo Zuniga kupitia Mtandao na Simu.
Ameeleza: “Tumeongea na Wahusika na kama mzazi nina wasiwasi! Meseji za kiwehu zimetufikia, vitisho vikubwa, na hata ubaguzi wa rangi!”
Aliongeza: “Sihofii kuhusu
mwanangu tu, pia kwa Mkewe na Binti wao! Baada ya hayo imebidi tupewe ulinzi na natumai hili ni la muda tu na litakwisha tuishi maisha yetu ya kawaida ya zamani!”
Camilo Zuniga alionyesha majonzi makubwa hasa alipokumbushia Neymar kumsamehe mwanawe: “Neymar alifuta lawama zote kwa mtoto wangu, mwanangu hakufanya kusudi. Hapendi vurugu na hana rekodi ya rafu mbaya! Mtoto wangu aliomba radhi mbele ya kadamnasi na kujieleza!”

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni