STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 21 Julai 2014

CHELSEA ZIARANI AUSTRIA NA SALAH LICHA KUITWA KWAO JESHINI!

MOHAMED-SALAHMCHEZAJI wa Chelsea Mohamed Salah yumo kwenye Kikosi cha Chelsea kitakachoenda Austria kwa Mazoezi licha ya kuwepo hofu anatakiwa arudi Nchini kwao Misri kutumikia Jeshi, kwa Mujibu wa Sheria, kwa Kipindi cha kuanzia Mwaka hadi Miaka Mitatu.
Klabu ya Chelsea imedokeza kuwa inazo taarifa kutoka Misri zinazodai Salah atalazimika kurudi kwao kwenda Jeshini na wameongea na Mchezaji huyo kuhusu suala hilo.
Lakini hadi sasa si Chelsea wala Salah ambae amepokea taarifa rasmi kuhusu wito huo.
Hii si mara ya kwanza kwa Chelsea kukumbwa kwa sakata la aina hii kwani waliwahi kuwa na Mchezaji kutoka Israel, Ben Sahar, ambae aliitwa Jeshini lakini pande zote zilikubaliana atumikie Jeshi mwishoni mwa Msimu kwa Wiki mbili.
Taarifa kutoka Misri zilidai kuwa Salah, mwenye Miaka 22 na ambae alijiunga na Chelsea Mwezi Januari Mwaka huu kutoka Basle ya Uswisi, aliruhisiwa kuishi Nchini Uingereza kwa sababu anajihusisha na Masomo lakini Wizara ya Elimu ya Juu ya Misri imefuta idhini hiyo na kumtaka arudi Misri mara moja ili
atumikie Jeshini kwa Mujibu wa Sheria kwa Kipindi cha kuanzia Mwaka Mmoja hadi Mitatu.
Kwenye Ziara ya huko Austria, Salah ataungana na Wachezaji wapya wa Chelsea Cesc Fabregas, Diego Costa na Filipe Luis, pamoja na Wachezaji wengine waliokuwa wakitumikia Nchi zao kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil akiwemo Sentahafu wa England, Gary Cahill.
Pia Kipa Petr Cech yumo kundini baada kurejea Mazoezini baada kupona Bega lake aliloumia mwishoni mwa Msimu.
Vile vile, Wachezaji wa Kimataifa wa Belgium, Straika Romelu Lukaku na Kipa Thibaut Courtois, ambao wote Msimu uliopita walikuwa nje ya Chelsea wakicheza kwa Mkopo, wamepangiwa kujiunga na Kikosi cha Chelsea kwa ajili ya tripu ya kwenda huko Holland kucheza na Vitesse Arnhem hapo Julai 30.
Wakati huo huo, Chelsea inamngojea Straika wao wa zamani, Didier Drogba, kuwajibu kama yupo tayari kurejea Klabuni hapo na kuwa Kocha-Mchezaji ingawa inaaminika Mchezaji huyo aliekuwa akichezea Galatasaray ya Uturuki anazo Ofa kutoka Juventus na Klabu kadhaa za MLS, Major League Soccer, hukO USA.
Chelsea
Ratiba/Matokeo Mechi za Kujipima Kabla Msimu mpya:
16 Julai Wycombe Wanderers 0 Chelsea 5 (Magoli: Bamford, Brown 2, Terry, Ivanovic)
19 Julai AFC Wimbledon 2 Chelsea 3, Kingsmeadow
23 Julai RZ Pellets WAC v Chelsea, Klagenfurt, Austria
27 Julai NK Olimpika Ljubljana v Chelsea, Ljubljana, Slovenia
30 Julai Vitesse Arnhem v Chelsea, Arnhem Stadium, Netherlands
3 Agosti Werder Bremen v Chelsea, Wesser Stadium, Germany
10 Agosti Ferencvaros v Chelsea, Albert Florian Stadium, Budapest, Hungary
12 Agosti Chelsea v Real Sociedad

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox