Hapa kazi tu mzee wangu!: Van Gaal akitabasamu wakati akimtazama Rooney ambaye pia alifurahi.
LOUIS van Gaal na wachezaji wake wa Manchester United wapo katika morali kubwa kwenye ziara yao nchini Marekani
.
.
Mholanzi huyo alionekana kucheka na
kutaniana na mshambuliaji wake, Wayne Mark Rooney, wakati wachezaji
wapya Luke Shaw na Ander Herera wakipata nafasi ya kuwajua wachezaji
wenzao.
Man United wamepigga kambi ya maandalizi
ya msimu mpya huko Marekani na sasa wanajiandaa na mechi ya kirafiki
jumatano ijayo dhidi ya LA Galaxy.
Van Gaal na Rooney walionaka kuelewana vizuri ambao mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England alikuwa anamtania bosi wake mpya.
Mwanzo mzuri: Kambi ya Man United ilionekana kuwa na furaha jumamosi mjini Los Angeles
Anasaka pumzi: mchezaji aliyesajiliwa kwa paundi milioni 30, Luke Shaw, kushoto, akifanya mazoezi na wenzake
Ander Herrera, kulia, alipata nafasi ya kuonesha ufiti wake kwa kocha wake na wachezaji wenzake
Herrera na Mata wakinyosha viungo
Kinda: Reece James ni miongoni mwa wachezaji wa Akademi walioitwa katika ziara ya Marekani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni